HATIMAYECHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAFANIKIWA KUAZIMISHA MAHAFALI YAKE YA 17 TOKEA KUANZISHWA KWA CHUO HICHO MWAKA 1988:
Chuo cha Uhasibu Arusha kimefanikiwa kuazimisha mahafali yake ya 17 tokea kilipoanzishwa kwa kuwatunuku wahitimu wapatao 1547 wa ngazi mbalimbali za Elimu ikiwa ni pamoja na ngazi ya
Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma), Shahada(Degree), Stashahada ya Uzamili (Post Graduate Diploma) na Shahada ya Uzamili (Degree ya Juu). Katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na maelfu ya wageni mbalimbali huku wakiongozwa na
Mgeni Rasmi Bw. Fadhili Mkulu makamu mkuu wa Mkoa wa Arusha pia kulishuhudiwa tukio la kukabidhiwa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao ya nadharia na vitendo pia ambapo
Yousa Youze na Agness Dominick wa ngazi ya Shahada walitia fora kwa kujinyakulia zawadi tatu tatu kwa kila mmoja.
Pia katika mahafali hayo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu
Prof. Johannes Monyo alimtambulisha Mwenyekiti mpya wa Baraza la Chuo kuwa ni
Bi. Rukia Adam aliyeteuliwa na Rais wa awamu ya nne
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua nafasi ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake.
Akitoa utangulizi wa awali katika mahafali hayo
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Campus ya Mwanza Dkt. Shishiwa alisema kuwa Chuo cha Uhasibu kimeanzishwa mnamo mwaka
1988 na hadi sasa kimefanikiwa kusambaza huduma yake katika mikoa minne kwa kuwa na Campus katika mikoa ya
Arusha (Main Campus), Dar-es-Salaam, Manyara (Babati Campus) na Mwanza.
Akizungumzia kuhusu idadi ya wanafunzi waliohitimu na mafanikio ya chuo Bi. Rukia Adam alisema kuwa Chuo kimefanikiwa kuongeza idadi ya wahitimu kutoka
1367 mwaka (2014) hadi 1547 mwaka huu (2015) ambapo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 180.
katika uchanganuzi wa wahitimu wa ngazi mbalimbali Bi.Rukia alisema wahitimu wa ngazi ya Astashahada ni 423, Stashahada 532, Shahada 468, Shahada ya Uzamili 117, Diploma ya juu ya Uchumi na Fedha (NTA Level 7) 2, Diploma ya Juu ya Fedha na Benki (NTA Level 7) 1, Advance Diploma ya Habari na Teknolojia 1, Advance Diploma ya Uhasibu 1, Astashahada ya Compyuta Sayansi (NTA Level 5) 1 na Astashahada ya Fedha na Benki (NTA Level 5) 1, ambapo jumla kuu ni
wahitimu 1547.
Akitoa maelezo kuhusu mipango ya Chuo Bi. Rukia Adam amesema kuwa Chuo kiko katika hatua za mwisho mwisho kuanza
Mafunzo ya Shada ya Kijeshi (Barchelor Degree in Military Art).
Akielezea matatizo yanayokikabili chuo na kuelekeza maombi yake kwa Mgeni Rasmi
Bi. Rukia alisema chuo kina
upungufu wa Mabweni ya wanafunzi, ukosefu wa Ukumbi mkubwa wa Mihadhara pamoja na tatizo la waajiri (Ajira) kutokana na Serikali kuzuia vibali vya ajira bila kusahau tatizo la Ruzuku ya Chuo kupunguzwa kutoka Millioni 120 mwaka jana hadiMillioni 70 jambo ambalo linasababisha shughuli za uendeshaji wa Chuo kuwa ngumu.
Habari katika picha:-
 |
| Baadhi ya wahitimu wakiwa katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Arusha yalipofanyikia Mahafali ya 17 ya Chuo hicho. (Picha na Amani Ly) |
Baadhi ya wahitimu pamoja nami (Elirinyo) katika picha ya pamoja (Picha na Amani Ly)
 |
| Baadhi ya wahitimu wakiwa katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Arusha yalipofanyikia Mahafali ya 17 ya Chuo hicho. (Picha na Amani Ly) |
 |
| Wahitimu katika chumba cha kuvalia Majoho "Martha & Jacky" (Picha Jackson Laizer) |
 |
| Baadhi ya wahitimu wakiwa katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Arusha yalipofanyikia Mahafali ya 17 ya Chuo hicho. (Picha na Amani Ly) |
 |
| Baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja. |
 |
| Baadhi ya wahitimu wakiwa katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Arusha yalipofanyikia Mahafali ya 17 ya Chuo hicho. (Picha na Amani Ly) | | |
@RINYO'S