Monday, 23 November 2015

CHADEMA YAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU YA MWANZA KUPINGA ZUIO LA KUMUAGA MWENYEKITI WA WA GEITA ALFONCE MAWAZO:

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hii leo kimefungua kesi katika mahakama kuu Jijini kupinga kuzuiwa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Geita, Alphonce Mawazo tamko lililotolewa na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza, ambapo Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo siku chache zilizopita iliagiza kwamba kusiwepo shughuli za kuaga mwili wa marehemu huyo kutokana na tatizo la ugonjwa wa kipindupindu kilichoibuka maeneo mbalimbali ya Jiji laMwanza. 

Hii leo Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallya wamefika Mahakama Kuu Mwanza na kufungua kesi na tayari  kesi hiyo imeshasomwa na kusikilizwa na Jaji Lameck Mlacha aliyeiahirisha hadi siku ya kesho ambapo mshtakiwa ambaye ni Mkuu wa Polisi  mkoa wa Mwanza na Wakili wa serikali watahitajika kuwasilisha utetezi wao.

Katika kesi hiyo CHADEMA iliwakilishwa na wanasheria watatu ambao ni John Mallya, James Milya na Paul Kipega ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambaye ni baba mdogo wa marehemu Mawazo.


Wakili wa CHADEMA John Mallya akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutoka katika mahakama kuu ya Jiji la Mwanza.

John Mallya ambaye ni mwanasheria wa Chadema aliyasema haya baada ya kutoka nje ya Mahakama 
 “Leo tumefungua kesi ya madai Mahakama kuu kwa hati ya dharura, mlalamikaji wa kesi ni baba mdogo wa marehemu Mawazo… Maombi yetu ni kupata ruhusa ya Mahakama ili kutengua zuio la Mkuu wa Polisi Mwanza kuhusu kuaga mwili wa marehemu Mawazo.”- John Mallya, Mwanasheria wa CHADEMA.

Pia John Mallya akiwa nje ya Mahakama aliyasema haya.
 “Kuna Mawakili watatu, kesi imesikilizwa leo upande mmoja na upande wa pili wa RPC Mwanza na Mwanasheria wa Serikali watasikilizwa kesho asubuhi… Jaji ameona jambo hili ni la dharura na linahusu mwili wa mtu aliyekaa mochwari kwa zaidi ya siku nane, amesema ataifanya kwa haraka.”-

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akiongea na wanahabari baada ya kutoka katika Mahakama Kuu ya Mwanza baada ya kufungua kesi.

Kuhusu mwendelezo wa kesi hiyo, Mahakama itaendelea nayo kesho Jumanne November 23 2015 na hiki ndio alichokisema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe 

 “Tumefungua madai ya kutaka kumuaga Kamanda wetu Mawazo, madai yetu yamepokelewa  Mahakama kuu, yamepangiwa Jaji na kesho asubuhi suala letu litaanza kusikilizwa"


@RINYO'S

No comments:

Post a Comment