Monday, 23 November 2015

SIMBA MTOTO YAPATA AJALI KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA :

Katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka basi la kampuni ya SIMBA MTOTO limepata ajali katika eneo la kwa Fundi katika mji mdogo wa TENGERU Jijini Arusha asubuhi ya leo, kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa chanzo ni mwendo wa dereva wa basi hilo la mkoani ambalo lilikua likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam, ambapo wanadai kuwa dereva huyo alikua anaovertake na wakati huo huo gari aina yaa fuso lililokuwa likielekea Arusha mjini likiovertake pia ndipo dereva wa Simba Mtoto alipofanya juhudi za kukwepa kugongana uso kwa uso na Fuso hiyo jambo ambalo lilisababisha basi hilo kupinduka.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakilitazama basi hilo lililopinduka (Picha na Elirinyo).

Hadi tunafika eneo la tukio mida ya saa 02:30  hatukuweza kukuta majeruhi wowote katika eneo la ajali, na mashuhuda wanasema kuwa majeruhi walikimbizwa Hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza na matibabu.
Basi la Simba Mtoto likiwa limepinduka katika eneo la TENGERU (Picha na Elirinyo)


Bado tunaendelea kutafuta mawasiliano kutoka kwa Kamanda mkuu wa usalama katika mkoa wa Arusha Liberatus Sabasi ili kuweza kujua hali za majeruhi na kuweza kujua kama kuna yeyote aliyepoteza maisha. 

Basi la Simba Mtoto kama linavyoonekana kwa mbele baada ya kupinduka (Picha na Elirinyo)



(Picha na Elirinyo)




@RINYO'S
CHADEMA YAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU YA MWANZA KUPINGA ZUIO LA KUMUAGA MWENYEKITI WA WA GEITA ALFONCE MAWAZO:

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hii leo kimefungua kesi katika mahakama kuu Jijini kupinga kuzuiwa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Geita, Alphonce Mawazo tamko lililotolewa na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza, ambapo Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo siku chache zilizopita iliagiza kwamba kusiwepo shughuli za kuaga mwili wa marehemu huyo kutokana na tatizo la ugonjwa wa kipindupindu kilichoibuka maeneo mbalimbali ya Jiji laMwanza. 

Hii leo Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallya wamefika Mahakama Kuu Mwanza na kufungua kesi na tayari  kesi hiyo imeshasomwa na kusikilizwa na Jaji Lameck Mlacha aliyeiahirisha hadi siku ya kesho ambapo mshtakiwa ambaye ni Mkuu wa Polisi  mkoa wa Mwanza na Wakili wa serikali watahitajika kuwasilisha utetezi wao.

Katika kesi hiyo CHADEMA iliwakilishwa na wanasheria watatu ambao ni John Mallya, James Milya na Paul Kipega ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambaye ni baba mdogo wa marehemu Mawazo.


Wakili wa CHADEMA John Mallya akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutoka katika mahakama kuu ya Jiji la Mwanza.

John Mallya ambaye ni mwanasheria wa Chadema aliyasema haya baada ya kutoka nje ya Mahakama 
 “Leo tumefungua kesi ya madai Mahakama kuu kwa hati ya dharura, mlalamikaji wa kesi ni baba mdogo wa marehemu Mawazo… Maombi yetu ni kupata ruhusa ya Mahakama ili kutengua zuio la Mkuu wa Polisi Mwanza kuhusu kuaga mwili wa marehemu Mawazo.”- John Mallya, Mwanasheria wa CHADEMA.

Pia John Mallya akiwa nje ya Mahakama aliyasema haya.
 “Kuna Mawakili watatu, kesi imesikilizwa leo upande mmoja na upande wa pili wa RPC Mwanza na Mwanasheria wa Serikali watasikilizwa kesho asubuhi… Jaji ameona jambo hili ni la dharura na linahusu mwili wa mtu aliyekaa mochwari kwa zaidi ya siku nane, amesema ataifanya kwa haraka.”-

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akiongea na wanahabari baada ya kutoka katika Mahakama Kuu ya Mwanza baada ya kufungua kesi.

Kuhusu mwendelezo wa kesi hiyo, Mahakama itaendelea nayo kesho Jumanne November 23 2015 na hiki ndio alichokisema Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe 

 “Tumefungua madai ya kutaka kumuaga Kamanda wetu Mawazo, madai yetu yamepokelewa  Mahakama kuu, yamepangiwa Jaji na kesho asubuhi suala letu litaanza kusikilizwa"


@RINYO'S
RAMSEY AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA ARSENAL:


Baada ya kukabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka hatimaye Klabu ya Arsenal imepata matumaini mapya baada ya kiungo wake Aaron Ramsey maarufu kwa jina la "Rambo" kurejea mazoezini hii leo katika viwanja vya mazoezi vya timu hiyo London Colney.

Aaron Ramsey akimiliki mpira katika mazoezi,

 Arsenal imejikuta katikaa wakati mgumu baada ya Jumamosi kupoteza wachezaji wawili tena muhimu wa kikosi cha kwanza ambao wote ni viungo wakabaji ambao ni Nahodha Mikael Arteta na Francis Couqulin ambaye anatazamiwa kuwa nje kwa kipindi kisichopungua miezi miwili hadi mitatu, Majeruhi hao wamefanya idadi ya majeruhi wa kikosi cha kwanza kufikia saba ambao ni Jack Wilshere, Danny Welbeck, Tomas Rosiscky, Theo Walcot na Alex Oxlade Chamberlain


Aaron Ramsey mazoezini.


 Kocha Arsena Prof. Arsenal Wenger anao wakati mgumu wa kuamua nani aanze katika eneo la kiungo wa ukabaji katika mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya  dhidi ya Dinamo Zagreb ya Ukraine ambapo atahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya kumi na sita bora.



Aaron Ramsey

@RINYO'S




 MAN UNITED YAPATA TUMAINI LA NYOTA WAKE KURUDI UWANJANI.

Klabu ya Manchester United inakabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuwa na lundo kubwa la wachezaji majeruhi hasa wa kikosi cha kwanza, lakini kocha wa klabu hiyo Louis Van Gaal ameelezea matumaini yake  ya wachezaji wake wawili wa kutumainiwa wa safu ya ushambuliaji Nahodha Wayne Rooney na Anthony Martial kuweza kurejea uwanjani katikati ya wiki hii katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford. Lakini kuna kiladalili za kuwakosa nyota wake wengine wa muhimu ambao ni kiungo Ander Herrera na beki Phil Jones ambao walipata majeraha hayo katika mechi dhidi ya Wartford ambapo United iliibuka na ushindi wa amagoli 2-1 katika uwanja wa Vicarage Road.

pia United inatarajia kumkosa James Willison mwenye tatizo la goti. Katika mchezo huo wa katikati ya wiki Man United wanahitaji ushindi ili waweze kusonga mbele katika hatua ya mtoano na 16 bora.

Kiungo wa United Ander Herrera akitolewa nje katika mechi dhidi ya Watford baada ya kupata majeraha

@RINYO'S