Baada ya kukabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka hatimaye Klabu ya Arsenal imepata matumaini mapya baada ya kiungo wake Aaron Ramsey maarufu kwa jina la "Rambo" kurejea mazoezini hii leo katika viwanja vya mazoezi vya timu hiyo London Colney.
![]() |
| Aaron Ramsey akimiliki mpira katika mazoezi, |
Arsenal imejikuta katikaa wakati mgumu baada ya Jumamosi kupoteza wachezaji wawili tena muhimu wa kikosi cha kwanza ambao wote ni viungo wakabaji ambao ni Nahodha Mikael Arteta na Francis Couqulin ambaye anatazamiwa kuwa nje kwa kipindi kisichopungua miezi miwili hadi mitatu, Majeruhi hao wamefanya idadi ya majeruhi wa kikosi cha kwanza kufikia saba ambao ni Jack Wilshere, Danny Welbeck, Tomas Rosiscky, Theo Walcot na Alex Oxlade Chamberlain
![]() |
| Aaron Ramsey mazoezini. |
Kocha Arsena Prof. Arsenal Wenger anao wakati mgumu wa kuamua nani aanze katika eneo la kiungo wa ukabaji katika mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dinamo Zagreb ya Ukraine ambapo atahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya kumi na sita bora.
![]() |
| Aaron Ramsey |
@RINYO'S



No comments:
Post a Comment