MAN UNITED YAPATA TUMAINI LA NYOTA WAKE KURUDI UWANJANI.
Klabu ya Manchester United inakabiliwa na wakati mgumu kutokana na kuwa na lundo kubwa la wachezaji majeruhi hasa wa kikosi cha kwanza, lakini kocha wa klabu hiyo Louis Van Gaal ameelezea matumaini yake ya wachezaji wake wawili wa kutumainiwa wa safu ya ushambuliaji Nahodha Wayne Rooney na Anthony Martial kuweza kurejea uwanjani katikati ya wiki hii katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford. Lakini kuna kiladalili za kuwakosa nyota wake wengine wa muhimu ambao ni kiungo Ander Herrera na beki Phil Jones ambao walipata majeraha hayo katika mechi dhidi ya Wartford ambapo United iliibuka na ushindi wa amagoli 2-1 katika uwanja wa Vicarage Road.
pia United inatarajia kumkosa James Willison mwenye tatizo la goti. Katika mchezo huo wa katikati ya wiki Man United wanahitaji ushindi ili waweze kusonga mbele katika hatua ya mtoano na 16 bora.
![]() |
| Kiungo wa United Ander Herrera akitolewa nje katika mechi dhidi ya Watford baada ya kupata majeraha |

No comments:
Post a Comment