CHUO CHA UHASIBU ARUSHA LEO HII KIMEKUMBWA NA SIMANZI KUBWA BAADA KUKUMBWA NA TANZIA YA VIJANA WAO WAWILI WA NGAZI YA SHAHADA (DEGREE).
Ulikua ni mchana mzuri wenye pilikapilika za hapa na pale huku ukihusisha pia maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambayo yaliambatana na tukio la kufanya usafi katika maeneo ya majumbani na kazini pia kama utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Lakini siku haikuweza kuisha vizuri katika Chuo cha Uhasibu Arusha kwani mnamo majira ya saa 11 jioni zilianza kusambaa taarifa za uvumi wa vifo vya wanafunzi wawili, huku wanafunzi wengi wakiwa katika kuhamaki na wakipambana huku na kule ili kuupata ukweli juu ya taarifa hizi ndipo taarifa rasmi zilipotufikia kuwa wanafunzi wawili wa ngazi ya Shahada wa chuo Cha Uhasibu Arusha wamepata ajali katika barabara ya Njiro - Arusha karibu na Kituo cha Mafuta cha BP. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa ajali hiyo ilihusisha Pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na wanafunzi hao pamoja na gari aina ya Land Cruizer, mashuhuda wanadai kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Marehemu Carthbet Massawe iligongana na gari hilo na kusababisha ajali hiyo kutokea ambayo ilisababisha Carthbet kupoteza maisha hapohapo huku mwenzake ambaye ni Emmanuel Robson Sabuni akiwahishwa Hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata lakini hata hivyo kwa taarifa tulizozipata kutoka Hospitali ni kuwa pia Emmanuel naye alifariki akiwa katika chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU).
Kwa kweli vifo hivi vimepokelewa kwa simanzi kubwa hapa chuoni huku wengi wakiwa bado hawaamini kwa taarifa wanazozipata kutoka kwa Magroup yao ya Whatssap ya madarasani. Vijana hawa wametutoka wakiwa bado wadogo sana huku wakikadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 23 na 25, Marehemu Emmanuel Sabuni alikua ni mwanafunzi wa Shahada ya TEHAMA (BIT) mwaka wa kwanza huku mwenzake ambaye ni Marehemu Carthbet Massawe akiwa ni mwanafunzi wa Shahada mwaka wa pili.
Wote walikua ni watumishi wa Mungu katika Fellowship ya ICF hapa chuoni na walikua katika maandalizi ya sherehe ya Kidini ya kuwakaribisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza (ICF FRESHERS) ambayo ilitarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Tarehe 12/12/2015.
![]() |
| Marehemu Emmanuel Sabuni katika enzi za uhai wake akiwa Madhabahuni. |
| Marehemu Emmanuel Sabuni akionekana katika moja ya Events alizoshiriki kuziandaa. |
![]() |
| Marehemu Carthbet Massawe katika enzi za Uhai wake. |
![]() |
| Marehemu Carthbet Massawe na Marehemu Emmanuel Sabuni katika picha ya pamoja, Bwana ametoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe. R.I.P Brothers. |
Share na wengine ili tuzidi kuwaombea wapendwa wetu hawa walazwe mahali pema peponi.
@RINYO'S









