LEO NI SIKU MUHIMU SANA KWA NCHI YETU KWA KUTIMIZA MIAKA 54 TANGU ILIPOJIPATIA UHURU WAKE MNAMO TAREHE 09/12/1961.
Lakini leo hii Rais wa Awamu ya Tano Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameamua watu wote waadhimishe siku hii kwa kufanya usafi katika makazi yao na maeneo yao ya kazi ili kuweza kukabiliana na Ugonjwa wa KIPINDUPINDU, zoezi hilo limeanza kutekelezwa asubuhi hii ya leo huku Mh. Rais akiliongoza kwa kufanya usafi katika eneo la Soko la Feri .
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Janeth akiongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Feri. |
![]() |
| Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongoza wananchi wa eneo chalinze kufanya usafi |
| Watangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm #TeamLeoTena wakiwa katika mavazi ya usafi kwa ajili ya kulitimiza agizo la Rais. (Dahuu, Musa Husein, Jose Mara, Ge Habibu nk.) |
![]() |
| Staa wa bongo Fleva Tundaman akiwa na Team Leo Tena ya Clouds wakifanya usafi eneo la Soko la Tandale. |
Pia Taasisi mbalimbali zimeonyesha kuunga mkono kauli ya Rais ya kufanya usafi ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya SEKOTOURE iliyoko jijini Mwanza pia Taasisi za Elimu ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM nacho kimeunga agizo la Mh. Rais kwa asilimia 100 na katika mbao zake za matangazo kulisomeka hivi.
| Tangazo katika mbao za matangazo za Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kama linavyoonekana. |
![]() |
| Mwanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefahamika kwa jina moja la Shangwe akivaa Gloves tayari kwa kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la kufanya usafi. |
![]() |
| Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya SEKOTOURE Jijini Mwanza wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi tayari kutekeleza agizo la Rais. |
Usisahau kutoa maoni yako juu ya maamuzi haya ya Rais na pia kuhusiana na mwitiko wa wananch katika eneo lako
@RINYO'S






No comments:
Post a Comment