TANZANIA RASMI OUT KATIKA MATUMAINI YA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018 URUSI:
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa kuamkia leo ilikumbana na dhahama baada ya kukubali kipigo cha aibu kutoka kwa timu ya taifa ya Algeria kwa kufungwa jumla ya magoli 7-0 na hivyo jumla kutolewa kwa idadi ya magoli 9-2 baada ya mchezo wa awali kutoka sare ya magoli 2-2.
http://elirinyouronu.blogspot.com/2015/11/tanzania-rasmi-out-katika-matumaini-ya.html
Wednesday, 18 November 2015
Wednesday 18/11/2015 (03:42 PM)
KOBE 201 WANASWA UWANJA WA KIMATAIFA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE WAKITAKA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI.
Akizungumzia tukio hilo Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru amesema kuwa kobe hao 201 walikamatwa uwanjani hapo na Askari wa Maliasili kwa ushirikiano na Askari wa usalama katika Uwanja wa ndege,wakiwa wamefungwa katika mabegi makubwa matano.
Watuhumiwa hao wa tukio hilo la usafirishaji wa Wanyamapori wametajwa kwa majina kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Tanga na Mohhamed Sulleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupenya katika mitambo ya ukaguzi katika Uwanja huo lakini Mbwa maalum (Sniffer Dogs) walisaidia kubaini uhalifu huo. Watuhumiwa hao kwa pamoja walithibitika kuwa na tiketi za kusafiria kwenda Malaysia.
Aidha katika tukio hilo Kobe wengine 103 walikamatwa wakiwa wametelekezwa katika eneo la Tabata.
http://elirinyouronu.blogspot.com/2015/11/18112015-0342-pm-kobe-201-wanaswa.html
@Rinyo
Subscribe to:
Comments (Atom)
