Sunday, 22 November 2015

BODI YA MIKOPO KWA ELIMU YA JUU (HESLB) YATOA TAARIFA MPYA KWA AMBAO HAWAJAAMBATANISHA BAADHI YA TAARIFA MUHIMU KWA BODI:


Taarifa inasomeka kuwa Bodi (HESLB) iko katika hatua za mwisho kuwapangia mikopo wanafunzi wote wa Elimu ya Juu walioomba kwa mwaka wa masomo wa 2015/2016. Na katika mchakato huo, Bodi imegundua kuwa wanafunzi waliotuma maombi wapatao 336 wanamapungufu katika Fomu zao za maombi ya Mkopo kwa kukosa nakala za Vyeti vya Kuzaliwa ili kubainisha na kuhalalisha Uraia/Utaifa wao.

Hivyo Bodi ya Mikopo (HESLB) inawahasa wote waliotuma maombi kwa mwaka wa masomo wa 2015/2016 kufika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo kwa Elimu ya Juu (HESLB) Kitalu Namba 8, Nyumba Namba 46 Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge - Dar es Salaam kwa ajili ya kuziwasilisha taarifa zao muhimu ikiwa ni pamoja na Nakala za Vyeti vyao vya Kuzaliwa . Ikumbukwe kuwa Bodi ilitoa siku kumi na nne (14) kwa wale wote ambao taarifa zao zilikua na makosa kuanzia Tarehe 27/08/2015 hadi Tarehe 11/09/2015 ili waweze kurekebisha makosa yote yaliyopatikana katika fomu zao za Maombi ya Mkopo.

Majina yote ya ambao taarifa zao hazijakamilika yanapatikana hapa.
Tarehe ya mwisho ya kukusanya hizo nakala za vyeti vya kuzaliwa ni Tarehe 30/11/2015 saa 11:00 Jioni. 

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Na kutafsiriwa na Elirinyo Uronu.

 Taarifa ya awali katika tovuti ya Bodi
 
NOTICE TO LOAN APPLICANTS TO SUBMIT COPIES OF CERTIFIED BIRTH CERTIFICATES:
:
The Higher Education Students’ Loans Board (HESLB) is finalizing allocation of students’ loans for the 2015/2016 Academic Year. In the process, we have identified 336 eligible applicants whose loan application forms miss birth certificates to authenticate their nationality.
 Therefore, HESLB hereby calls upon loan applicants for academic year 2015/2016 whose names are appended herewith to physically come to HESLB offices on Plot No. 8, Block No. 46 Sam Nujoma Road, Mwenge - Dar es Salaam to submit their certified copies of birth certificates.  It should be remembered that, the Board had earlier on given loan applicants fourteen days starting from 27th August, 2015 to 11th September, 2015 to rectify anomalies found in their application forms.
 Names of concerned applicants can be accessed here
The deadline for submission of certified birth certificates is 30th November, 2015 at 5.00pm.

 

Issued by:
  Executive Director
  HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD



@RINYO'S
RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI AUKWAA UKUU WA CHUO KIKUU CHA KAMPALA DAR-ES-SALAAM:


Usisahau ku-share na wenzako:


Kama ulikua haujui inabidi uanze kujua kuwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Ali Hassan Mwinyi kwa sasa ni mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International kilichopo jijini Dar-es-Salaam katika eneo la Gongo la Mboto, Chuo hicho kwa sasa kimefanikiwa kupata Leseni yakuweza kujiendesha chenyewe badala ya kuwa Chuo kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Kampala International kilichopo nchini Uganda, hayo aliyatanabaisha Mkuu huyo wa chuo Mh. Ali Hassan Mwinyi katika Mahafali ya Tatu ya Chuo hicho.


Mkuu wa Chuo cha Kampala International Mh. Ali Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Tanzania akiwa pamoja na wakuu wengine wa bodi ya Chuo pamoja na Wahadhiri wakijongea katika viwanja vya Mahafali ya 3 ya Chuo hicho.



Mkuu wa Chuo cha Kampala International Mh. Ali Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Tanzania akiwa pamoja na wakuu wengine wa bodi ya Chuo pamoja na Wahadhiri wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa unaimbwa. katika Mahafali ya 3 ya Chuo hicho.

 Katika Hotuba yake Mh.Ali Hassan Mwinyi aliwahimiza Watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali yatolewayo katika Chuo hicho cha Kampala International kilichopo Dar-es-Salaam katika eneo la Gongo la Mboto. Akihutubia katika hafla hiyo ya kuwatunuku wahitimu wa ngazi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashahada ya fani mbalimbali za Taaluma alisema kuwa chuo hicho kinatoa Elimu bora kwa fani mbalimbali kwa hiyo akawataka Watanzania wachangamkie fursa hiyo ya kupata Elimu bora na kuongeza ujuzi na maarifa katika chuo hicho ili waweze kuwa na ushindani katika soko la Ajira na hata kuweza kujiajiri wenyewe.

Pia Mkuu huyo wa Chuo amewapongeza wawekezaji hasa waliweza kuwekeza katika Sekta ya Elimu na kuiomba Serikali iweze kushirikiana nao vyeema ili Taifa liweze kupata na kuongeza wataalamu katika fani mbalimbali.


Mkuu wa Chuo cha Kampala International Mh. Ali Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Tanzania akitoa Hotuba wakati wa hafla ya Mahafali hayo hiyo siku ya jana Tarehe 21/11/2015.






































@RINYO'S


WABUNGE WA UKAWA WACHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUISAIDIA FAMILIA YA MAREHEMU ALFONCE MAWAZO:


Baadhi ya Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakichangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia familia ya Mawazo.(Picha na Chadema Blog).

WABUNGE wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamepanga kuchangisha kiasi cha Sh. 33.9 milioni kwa ajili ya kusaidia familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa Geita, Alfonce Mawazo aliyeuawa hivi karibuni na watu wasiojulikana huko Geita.

Fedha, hizo zimepatika baada ya wabunge 113 wa Ukawa kuchangishana kiasi Sh. 300,000 kila mmoja ambazo zitakabidhiwa kwa familia ya Mawazo ambaye ameuawa kikatili na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana.

Mwenyekiti wa Chadema – Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Aikaeli Mbowe alisema hayo mjini Dodoma baada ya kuulizwa na vyombo vya habari kuhusu maandalizi ya mazishi ya kada huyo ambaye anatajwa kuwa shujaa katika mapambado ya kutafuta ukombozi Ukawa.

Mbowe amesema licha ya kwamba Mawazo alikuwa mwanachama wa Chadema lakini pia alishiriki vyema katika ukombozi ndani ya Ukawa kwa kutetea masilahi ya Watanzania kwenye mkoa wake wa Geita pamoja na mikoa mingine nchini ikiwa ni pamoja na Arusha na hata Mwanza.


Freeman Mbowe alisema, nanukuu:-
 

“Kwa ujumla wetu wabunge takribani 113 tumekubaliana kuchanga kiasi cha Sh. 300,000 kila mmoja kwa ajili ya kuiwezesha familia yake ambayo ameiacha. Kumbuka kwamba Mawazo amepigania masilahi ya Watanzania wengi katika mkoa wake wa Geita lakini pia katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Hivyo tunalazimika kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wetu wa Ukawa"

Hata hivyo, Mbowe amesema inasikitisha kuona jeshi la polisi linavyotumiwa vibaya na kujikuta linafanya kazi za siasa badala ya kusimamia ulinzi na usalama wa raia na hii ni baada ya Jeshi hilo la Polisi kuzuia shughuli za Ibada ya kuuaga mwili wa Kamanda Alfonce Mawazo.


Mbowe alisema:-

“Leo (juzi), baada ya viongozi wa Mji wa Mwanza kupambana vikali na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, aliwaambia viongozi wa Chadema kuwa intelejensia imeonesha kuwa, iwapo watafanya mkusanyiko wa ibada kuna uwezekano wa kuzuka machafuko. Baada ya kupata taarifa hizo nilipata kuzungunza na IGP na kuniahaidi kunipatia majibu lakini hadi sasa sijafanikiwa kupata majibu lakini jambo lingine na la ajabu ni pale ambapo wamegeuza kibao na kusema hakuna kufanya ibada kwani kwa sasa kuna ugonjwa wa kipindupindu hivyo hakuna mkusanyiko,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema lazima Watanzania watambue kuwa serikali inatumia vibaya vyombo vyake vya dola kuzuia wapinzania wasifikishe ujumbe wao kwa jamii, imefikia hatua ya kuzuia hata watu kuwazika wafuasi wao. 


@RINYO'S

BAADA KIPIGO CHA 7-0 MKWASA AWACHOKOZA ALGERIA NA SASA KUSHITAKIWA FIFA:

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania  Charles Boniface Mkwasa


Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa atajikuta katika wakati mgumu baada ya kuwatuhumu wananchi wa Algeria kuwa ni wabaguzi wa rangi.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanasoka wa Algeria, Ahmed Boudry ameamua kumfungulia mashitaka Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa.
Kulingana na habari kutoka kwenye tovuti ya Le Buteur, Boudry amesema wamekerwa kupita kiasi na kauli ya Mkwasa kwamba raia wa Algeria ni wabaguzi wakubwa wa rangi, hivyo wameamua rasmi kumfungulia mashitaka katika  Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Ahmed Boudry alisema kuwa nanukuu.

 “Mkwasa aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hata kabla ya mechi ambayo Tanzania ilifungwa bao saba. Tunaamua kumfikisha Fifa kwa kuwa amewadhalilisha raia wote wa Algeria wakiwemo wachezaji".

Pia aliongeza kuwa:-

“Mkwasa hakuwa na ushahidi, Tanzania imekuja hapa zaidi ya mara moja na hatujawahi kupata malalamiko ya ubaguzi wa rangi, vipi yeye Mkwasa aseme hayo?” alihoji kiongozi huyo.

Kabla ya kauli yake hiyo, vyombo vingi vya habari vya Algeria vilizungumzia suala la Mkwasa kusema Waalgeria ni wabaguzi wa rangi. Vyombo hivyo vya habari vya Algeria ikiwemo mitandao inayotumia lugha ya Kifaransa vilimshambulia Mkwasa kwa madai amewakashifu Waalgeria.
Algeria iliing’oa Stars kwa kuifunga mabao 7-0 katika mechi ya marudiano kufuzu Kombe la Dunia 2018 mjini Bilda.  Stars imeaga michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya mabao 9-2 kwani awali ilitoka sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa.
LIGI MAARUFU DUNIANI ZAZIDI KUSHIKA KASI HUKU BAADHI YA VIGOGO VIKIANGUKIA PUA:

Ligi yenye wapenzi wengi zaidi ulimwenguni na yenye umaarufu kuliko zote ni Ligi kuu ya England  (EPL) ikifatiwa kwa karibu na Ligi   kuu ya Spain (La Liga). Wikiendi hii kulikua na mitanange miwili mikubwa iliyovuta hisia za wapenzi wengi wa soka kote ulimwenguni, ambayo ni mtanange kati ya Manchester City dhidi ya Liverpool na mtanange kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona kule Spain.

Mitanange hiyo ilitoa matokeo ya ajabu kwa siku ya jana kinyume na matarajio ya wengi ambapo kati mpambano kati ya Manchester City Vs Liverpool, Man City iliyokuwa uwanja wao wa nyumbani wa Etihad ilikubali kichapo cha fedhea kwa kufungwa jumla ya magoli 4-1, huku Real Madrid ikikubali kutandikwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Santiago Bernabeu kwa jumla ya magoli 4-0.

 Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa City Liverpool ndiyo iliyokuwa ya kwanza kujipatia goli mnamo dakika ya 8 baada ya beki wa Man City Eliquim Mangala kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa, mnamo dakika ya 23 kiungo mshambuliaji wa Liverpool aliye katika kiwango cha juu Phillipe Coutinho aliiongezea Liverpool goli la pili kama hiyo haitoshi Roberto Firmino kwa ushirikiano mzuri na Mbrazil mwenzake Coutinho aliipatia Liverpool goli la tatu katika dakika ya 32 na kuzidi kulididimiza jahazi la wenyeji City.
Roberto Firmino akishangilia na wachezaji wenzake goli la Tatu aliloifungia Liverpool.
 Huku mashabiki wakitegemea kipindi cha kwanza kitaisha kwa magoli hayo matatu ya Liverpool Sergio Kun Aguero aliipatia Man City goli la kufutia machozi mnamo dakika ya 44 kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Liverpool Mbeligiji Simon Mignollet.

Sergio Kun Aguero akiifungia Man City goli la kufutia machozi.

 Manchester City walirejea uwanjani kipindi cha pili wakiwa na nguvu kubwa ya kutaka kusawazisha magoli lakini hata hivyo juhudi zao ziligonga mwamba kutokana na umakini wa walinzi wa Liverpool wakiongozwa na Martin Skrtel.

Mnamo dakika ya 81 beki kisiki Martin Skrtel alipigilia msumari wa mwisho kwa kuiandikia Liverpool goli la nne na la mwisho katika mchezo huo kwa shuti kali lililomuacha kipa Joe Hart asijue la kufanya. Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji 54,444 ulishudia kiungo mshambuliaji wa Liverpool Mbrazil Phillipe Coutinho akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Martin Skrtel akipiga shuti kuifungia Liverpool goli la nne



Beki Martin Skrtel akishangilia baada ya kufunga goli la nne na kufanya ubao kusomeka Man City 1-4 Liverpool.



Wachezaji wa Man City wakiwa katika nyuso za majonzi baada ya kupokea kipigo cha magoli 4-1 kutoka kwa Liverpool.


 Katika michezo mingine ya mapema ya EPL Arsenal The Gunners ilijikuta ikiangukia pua baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 ikiwa ugenini kwa West Bromwich Albion, ambapo pia katika mchezo huo ilishuhudia ikimpoteza kiungo wake mkabaji Francis Couqulin pia ikishuhudi wakijifunga baada ya kiungo wake na Nahodha Mikel Arteta kujifunga katika harakati za kuokoa, kama hiyo haitoshi pia Arsenal ilikosa nafasi ya kujipatia goli la kusawazisha baada ya Santiago Carzola kukosa mkwaju wa penalti. Pia katika michezo iliyopigwa hiyo jana Manchester United ilipata ushindi wa magoli 2-1 baada ya kuifunga Wartford, Chelsea nayo ilifanikiwa kujipatia ushindi wake wa kwanza katika ligi baada ya kupoteza michezo saba mfululizo, na hiyo jana ilifanikiwa kujipatia ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Norwich City.

@RINYO'S