Ligi yenye wapenzi wengi zaidi ulimwenguni na yenye umaarufu kuliko zote ni Ligi kuu ya England (EPL) ikifatiwa kwa karibu na Ligi kuu ya Spain (La Liga). Wikiendi hii kulikua na mitanange miwili mikubwa iliyovuta hisia za wapenzi wengi wa soka kote ulimwenguni, ambayo ni mtanange kati ya Manchester City dhidi ya Liverpool na mtanange kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona kule Spain.
Mitanange hiyo ilitoa matokeo ya ajabu kwa siku ya jana kinyume na matarajio ya wengi ambapo kati mpambano kati ya Manchester City Vs Liverpool, Man City iliyokuwa uwanja wao wa nyumbani wa Etihad ilikubali kichapo cha fedhea kwa kufungwa jumla ya magoli 4-1, huku Real Madrid ikikubali kutandikwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Santiago Bernabeu kwa jumla ya magoli 4-0.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa City Liverpool ndiyo iliyokuwa ya kwanza kujipatia goli mnamo dakika ya 8 baada ya beki wa Man City Eliquim Mangala kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa, mnamo dakika ya 23 kiungo mshambuliaji wa Liverpool aliye katika kiwango cha juu Phillipe Coutinho aliiongezea Liverpool goli la pili kama hiyo haitoshi Roberto Firmino kwa ushirikiano mzuri na Mbrazil mwenzake Coutinho aliipatia Liverpool goli la tatu katika dakika ya 32 na kuzidi kulididimiza jahazi la wenyeji City.
![]() |
| Roberto Firmino akishangilia na wachezaji wenzake goli la Tatu aliloifungia Liverpool. |
![]() |
| Sergio Kun Aguero akiifungia Man City goli la kufutia machozi. |
Manchester City walirejea uwanjani kipindi cha pili wakiwa na nguvu kubwa ya kutaka kusawazisha magoli lakini hata hivyo juhudi zao ziligonga mwamba kutokana na umakini wa walinzi wa Liverpool wakiongozwa na Martin Skrtel.
Mnamo dakika ya 81 beki kisiki Martin Skrtel alipigilia msumari wa mwisho kwa kuiandikia Liverpool goli la nne na la mwisho katika mchezo huo kwa shuti kali lililomuacha kipa Joe Hart asijue la kufanya. Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji 54,444 ulishudia kiungo mshambuliaji wa Liverpool Mbrazil Phillipe Coutinho akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
![]() |
| Martin Skrtel akipiga shuti kuifungia Liverpool goli la nne |
![]() |
| Beki Martin Skrtel akishangilia baada ya kufunga goli la nne na kufanya ubao kusomeka Man City 1-4 Liverpool. |
![]() |
| Wachezaji wa Man City wakiwa katika nyuso za majonzi baada ya kupokea kipigo cha magoli 4-1 kutoka kwa Liverpool. |
Katika michezo mingine ya mapema ya EPL Arsenal The Gunners ilijikuta ikiangukia pua baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 ikiwa ugenini kwa West Bromwich Albion, ambapo pia katika mchezo huo ilishuhudia ikimpoteza kiungo wake mkabaji Francis Couqulin pia ikishuhudi wakijifunga baada ya kiungo wake na Nahodha Mikel Arteta kujifunga katika harakati za kuokoa, kama hiyo haitoshi pia Arsenal ilikosa nafasi ya kujipatia goli la kusawazisha baada ya Santiago Carzola kukosa mkwaju wa penalti. Pia katika michezo iliyopigwa hiyo jana Manchester United ilipata ushindi wa magoli 2-1 baada ya kuifunga Wartford, Chelsea nayo ilifanikiwa kujipatia ushindi wake wa kwanza katika ligi baada ya kupoteza michezo saba mfululizo, na hiyo jana ilifanikiwa kujipatia ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Norwich City.
@RINYO'S





No comments:
Post a Comment