![]() |
| Baadhi ya Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakichangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia familia ya Mawazo.(Picha na Chadema Blog). |
WABUNGE wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamepanga kuchangisha kiasi cha Sh. 33.9 milioni kwa ajili ya kusaidia familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa Geita, Alfonce Mawazo aliyeuawa hivi karibuni na watu wasiojulikana huko Geita.
Fedha, hizo zimepatika baada ya wabunge 113 wa Ukawa kuchangishana kiasi Sh. 300,000 kila mmoja ambazo zitakabidhiwa kwa familia ya Mawazo ambaye ameuawa kikatili na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana.
Mwenyekiti wa Chadema – Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Aikaeli Mbowe alisema hayo mjini Dodoma baada ya kuulizwa na vyombo vya habari kuhusu maandalizi ya mazishi ya kada huyo ambaye anatajwa kuwa shujaa katika mapambado ya kutafuta ukombozi Ukawa.
Mbowe amesema licha ya kwamba Mawazo alikuwa mwanachama wa Chadema lakini pia alishiriki vyema katika ukombozi ndani ya Ukawa kwa kutetea masilahi ya Watanzania kwenye mkoa wake wa Geita pamoja na mikoa mingine nchini ikiwa ni pamoja na Arusha na hata Mwanza.
Freeman Mbowe alisema, nanukuu:-
“Kwa ujumla wetu wabunge takribani 113 tumekubaliana kuchanga kiasi cha Sh. 300,000 kila mmoja kwa ajili ya kuiwezesha familia yake ambayo ameiacha. Kumbuka kwamba Mawazo amepigania masilahi ya Watanzania wengi katika mkoa wake wa Geita lakini pia katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Hivyo tunalazimika kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wetu wa Ukawa"
Hata hivyo, Mbowe amesema inasikitisha kuona jeshi la polisi linavyotumiwa vibaya na kujikuta linafanya kazi za siasa badala ya kusimamia ulinzi na usalama wa raia na hii ni baada ya Jeshi hilo la Polisi kuzuia shughuli za Ibada ya kuuaga mwili wa Kamanda Alfonce Mawazo.
Mbowe alisema:-
“Leo (juzi), baada ya viongozi wa Mji wa Mwanza kupambana vikali na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, aliwaambia viongozi wa Chadema kuwa intelejensia imeonesha kuwa, iwapo watafanya mkusanyiko wa ibada kuna uwezekano wa kuzuka machafuko. Baada ya kupata taarifa hizo nilipata kuzungunza na IGP na kuniahaidi kunipatia majibu lakini hadi sasa sijafanikiwa kupata majibu lakini jambo lingine na la ajabu ni pale ambapo wamegeuza kibao na kusema hakuna kufanya ibada kwani kwa sasa kuna ugonjwa wa kipindupindu hivyo hakuna mkusanyiko,” amesema Mbowe.
Mbowe amesema lazima Watanzania watambue kuwa serikali inatumia vibaya vyombo vyake vya dola kuzuia wapinzania wasifikishe ujumbe wao kwa jamii, imefikia hatua ya kuzuia hata watu kuwazika wafuasi wao.
@RINYO'S

No comments:
Post a Comment