HATIMAYE TANZANIA YAFANIKIWA KUMPATA WAZIRI MKUU MPYA:
Katika siku nzima ya Ijumaa ya Tarehe 19/11/2015 habari kubwa iliyokuwa imetapakaa nchini ni habari kuhusu mchakato wa kumpata waziri mkuu wa serikali ya awamu ya ttano ambayo itakua chini ya Mh. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa awmu ya tano.
Katika kikao cha Bunge la Jamuhuri kilichoketi jina la Majaliwa Kassim Majaliwa liliwasilishwa baada ya kupendekezwa na Rais na hii ilikua ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi ambao walikuwa wakieneza tetesi huku na kule mara wakisema atakuwa huyu na wengine wakisema atakuwa yule. Majaliwa Kassim Majaliwa ambaye ni Mbunge wa Ruangwa alipigiwa na Wabunge ili kuuthibitisha uteuzi wake ambapo alifanikiwa kupitishwa kwa kishindo kwa kupata kura zaidi ya 250 ambayo ni sawa na asilimia 73% ya kura zote, na hivyo kutangazwa rasmi na Spika wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Job Ndugai kuwa Waziri Mkuu Mpya wa Tanzania.
 |
| Waziri Mkuu mpya wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kama anavyoonekana katika picha akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza baada ya uteuzi. |
Aidha katika hatua nyingine Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamali Malinzi amemtumia salamu za pongezi Mh. Majaliwa kupitia akaunti yake
Tweeter kwa uteuzi huo kwani ni mdau mkubwa wa mpira wa miguu hapa nchi huku akiwa na Leseni ya Daraja B ya ukocha kutoka katika shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).
WASIFU WA MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA:
| Vijalizo vya Jina | Mhe. |
|
| Jina la Ukoo: | Majaliwa |
| Jina la Kwanza: | Kassim |
| Jina la Kati: | Majaliwa |
| Tarehe ya Kuzaliwa: | 1960-12-22 |
| Mahali Alipozaliwa: |
|
| Hali ya Ndoa: | Nimeoa |
| Kundi: | Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano |
| Jinsia: | M |
| Simu ya Ofisi: | - |
| Simu ya mkononi: | 785205910 |
| Barua pepe: | majaliwa.kasimu@yahoo.com |
| Anuani: | P.O.Box 51,
Ruangwa |
|
| Elimu |
| Toka | Hadi | Jina la Shule/Chuo | Cheti |
|
| 1970 | 1976 | Mnacho Primary School | cheti cha Elimu ya Msingi |
| 1977 | 1980 | Kigonsera Secondary School | CSEE |
| 1991 | 1993 | Mtwara Teachers College | - |
| 1994 | 1998 | University of Dar es Salaam | Bachelor Degree |
| 1999 | 1999 | Storckolm University | PGDP |
|
|
| Mafunzo Mengineyo |
| - |
|
| Uzoefu |
| Toka | Hadi | Jina la Mwajiri | Ngazi/Nyazifa |
|
| 2010 | 2014 | - | MB |
| 2006 | 2010 | PM | Mkuu wa Wilaya |
| 2001 | 2006 | PS-CWJ | Katibu Mkoa |
| 2001 | 2001 | PS-CWJ | Katibu Wilaya |
| 1988 | 2000 | PS-Moec | Mkufunzi |
| 1984 | 1986 | TD-Lindi Council | Mwalimu |
|
@RINYO'S