TOP FIVE HABARI KUBWA ZA WIKI (IAA):
1: KUZINDULIWA KWA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA IAASO:
Tarehe 19/01/2016.
Kampeni rasmi za uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri mkuu zinazinduliwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha baada ya kukwamishwa na pingamizi lililokuwa limewekwa kwa mmoja wa wagombe mmojawapo wa kiti cha Urais Ndg. Reginald Massawe, ambapo alifanikiwa kushinda pingamizi hilo ambalo lilitolewa maamuzi yake mnamo siku ya Jumatatu Tarehe 18/01/2016 kwenye mishale ya saa Mbili usiku.
![]() |
| Mgombea wa Urais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha Bw. Reginald Massawe aliyekuwa amewekewa pingamizi hapo awali. |
2: PICHA ZA WAGOMBEA ZAWEKWA NA KUSAMBAZWA KWENYE MBAO MBALIMBALI ZA MATANGAZO:
(A.) Wagombea watatu wa ngazi ya Urais ambao ni MASSAWE REGNALD, ZUBERI MAHAMUDU na SAID:
![]() ![]() |
| Wagombea wa nafasi ya Urais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO). |
(B.) Wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais walikua ni MWIGUNE ESTER na KATUNZI FARIDA.
![]() ![]() |
| Wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) |
(C.) Wagombea wa nafasi ya Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) walikua ni ELIBARIKI BONIFACE, MBOTOYO EMMANUEL na ALFA MAHAMED.
![]() ![]() ![]() |
| Wagombea wa nafasi ya Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) |
3: KAMBI MBILI ZAIBUKA RASMI WAKATI WA KAMPENI:
Kweli wahenga walisema siku zote maji hujitenga na mafuta, na ndivyo ilivyokuwa kwenye kampeni za uchaguzi huu ambapo kuliibuka kambi mbili zilizoibua ushindani mkubwa katika uchaguzi huu haswa wakati wa kampeni ambapo kambi hizo zilikua ni kambi ya Team Massawe na Team Mahamudu ambapo hizi kambi mbili zilihusisha viongozi wa nyazifa zote tatu, namaanisha nyadhifa za Urais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Huku kambi ya Team Massawe ikiwa na Massawe mwenyewe, Ester Mwigune na Elibariki Boniface, Upande wa pili wa Team Mahamudu ulikua na Mahamudu Zuberi, Katunzi Farida na Mbotoyo Emmanuel.
![]() |
| Kambi ya Massawe Regnald |
![]() ![]() ![]() |
| Kambi ya Mahamudu Zuberi |
Kambi ya Mahamudu Zuberi ilikua ikijinadi kwa Ilani yao inayosema "You Are the Best, Choose the Best, Hope for All" wakimaanisha "Wewe ni Bora, Chagua kilicho Bora, Tumaini la Wote".
Wagombea wawili pekee ndio waliokuwa binafsi na walikua na kambi huru ambao ni Said Mgombea wa nafasi ya Rais na Alfa Mohamed aliyekua mgombea wa nafasi ya Waziri Mkuu.
Kampeni za uchaguzi huo wa viongozi wa IAASO zilizidi kushika kasi kati siku ya pili ambayo ni Jumatano ambapo pia zilikumbwa na vikwazo vya hapa na pale ikiwamo pia mvua iliyozuia wagombea kutoka darasa moja hadi jingine huku pia madarasa kuwa na wanafunzi wachache.
5: UCHAGUZI WAFANYIKA NA MATOKEO YATANGAZWA:
Tarehe 22/01/2016.
Siku ya Ijumaa ya Tarehe 22/01/2016 ndo siku iliyokuwa muhimu baada ya kampeni zilizodumu kwa takribani masaa 72. Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha walitakiwa kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wao wa serikali ya wanafunzi ya wanafunzi (IAASO), Siku ilikua imetulia sana huku kukiwa na pitapita za hapa na pale pia kukihusisha vikundi vidogo vidogo vya wanafunzi hapa na pale wakitoa mitazamo tofauti juu ya wagombea baada ya kupiga kura zao.Zoezi liliendelea hivyo hadi saa 10:30 Jioni ambapo vituo vilisitisha zoezi la kupiga kura na kuanza zoezi jipya la kuhesabu kura na kisha kuzipeleka kura katika kituo kikuu ambapo yalifanyika Majumuisho.
Huku watu wengi wakiwa na hamu kubwa kusikia matokeo na kujua kipi hasa kimetokea ndipo Mwenyekiti wa Tume alipotoka na kutangaza matokea ambayo yalionyesha kuwa Bw. Massawe Regnald aliibuka mshindi wa kiti cha Urais kwa kupata jumla ya Asilimia 77.7% ya kura zote zilizopigwa huku akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu Bw. Mahamudu Zuberi aliyejipatia Asilimia 21.58%.
Kwa upande wa Makamu wa Rais Mwigune Ester aliibuka mshindi kwa kujipatia ushindi wa Asilimia 71.07% huku mpinzani wake Katunzi Farida akijipatia Asilimia 28.92%.
Katika matokeo ya Waziri Mkuu kulikua na mchuano kidogo ambapo wagombea watatu waligawana kura na mwisho Bw. Elibariki Boniface aliibuka kidedea kwa Asilimia 59.75% huku mpinzani wake wa karibu Bw. Alfa Mohamed akipata Asilimia 27.29% na Mbotoyo Emmanuel akipata Asilimia 12.95%.
![]() |
| Matokeo ya Uchaguzi wa IAASO katika Picha (Picha na Elirinyo) |
JICHO LA MWEWE LA MPEKUZI RINYO:
MAPUNGUFU:
Kwa kweli uchaguzi huu umegubikwa na Mapungufu kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na
- Mwamko mdogo wa wapiga kura
Chuo cha Uhasibu kwa makadirio ya chini kabisa kina Idadi ya wanafunzi Takribani 3000 (Elfu tatu) hayo ni makadirio ya chini kabisa lakini idadi ya waliopiga kura jumla ni wanafunzi 1455. unaona ni kwa namna gani mwamko ni mdogo kiasi cha kutokufikia hata nusu ya makadirio.
- Tume kutokuwa na karatasi maaalum za kufanyia mjumuisho wa matokeo. Kwa jicho langu la mwewe nimeweza kugundua kabisa karatasi iliyotumika kujumuishia matokeo ya ujumla kabisa ilitengenezwa kwa kutumia Rula na Kalamu jambo ambalo ni hatari sana kwani mtu yeyote anaweza akatengeneza matokeo kisha akabandika kabla ya Tume.
- Tume kutokuchukua hatua mathubuti kwa kampeni chafu na za kiholela zinazofanyika nje na ndani ya chuo, jambo ambalo linaweza kuchangia machafuko chuoni na hata kupandikiza chuki za kudumu baina ya wanafunzi.
- Jicho la Mwewe pia limeona mapungufu katika muda wa kufanya kampeni
MAONI YA MPEKUZI RINYO:
- Tume zijazo lazima zianzishe utaratibu mpya au mfumo mpya wa kuwagusa kila wanafunzi na kuwajengea hamasa za kushiriki katika uchaguzi hasa wanaume.
- Tume inatakiwa kuandaa na kuzifuatilia sheria na kanuni zake vizuri ili kuweza kuepuka vitendo vya kampeni chafu dhidi ya wagombea
@RINYO'S


























