ANGALIA PICHA ZA RAIS DR. MAGUFULI AKISHONA NGUO KWA CHEREHANI...!!!
Rais
Dr. John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia
Cherehani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya
kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali na watumishi wake wa Ikulu
jijini Dar es salaam jana Januari 20, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wabunge, bungeni mjini
Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto
ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kahilillah
Wabunge, Jenista Mhagama wa Peramiho (kushoto) na January Makamba wakiteta katika mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerge Masaju akitoa mada katika mkutano wa wabunge , bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016.
Spika
wa Bunge Job Ndugai akizungumza kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkutano wa
Wabunge, Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kufungua mkutano huo bungeni mjini
Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas
Kashilillah.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nasari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016.
3: RAIS MH. MAGUFULI ATINGA MAGWANDA YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) AKIWA JIJINI ARUSHA:
Tarehe 22/01/2016.
Tukio hili lilizua gumzo kubwa sana mitandaoni na hii ni baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kuamua kuvaa mavazi ya kijeshi alipokua kwenye ziara yake Jijini Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza
kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo
Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani
pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo
Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akisoma bango alilokabidhiwa na mwananchi mmoja
katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech.
Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais
Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani
Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General
Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani
lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis
Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo
Medan.
4: ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA BARA LA AFRIKA DR. SALIM AHMED SALIM AZINDUA KITABU:
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi
katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim
Ahmed Salim: Son of Afica),akimzungumzia historia iliyotukuka ya Dkt.
Salim Ahmed Salim, kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho.
Dkt.
Salim Ahmed Salim, akitoa maneno ya Shukrani kwa heshima aliyopewa kwa
Mwandishi wa kitabu hicho lakini kwa wadau wote waliohudhuria hafla hiyo
ya uzinduzi wa kitabu chake. Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Katikati), akiwa na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Dkt. Salim.
5: RAIS MH. MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JESHI HUKO MONDULI:
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli
Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo
cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo
Peter Massao.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya
Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa
cheo cha Luteni Usu.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni
kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
gwaride lililokuwa likipita mbele yake kutoa heshima.
Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni
rasmi Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli .















No comments:
Post a Comment