Wednesday, 2 December 2015

BREKING NEWSSS...............................
TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAMUZIKI WA ZAMANI KASONGO MPINDA CLYTON..


Jioni ya leo tumepokea taarifaza kifo cha mzee wetu huyu Kasongo Mpinda baada ya kuugua kwa muda mrefu, Kasongo atakumbukwa sana na vijana wengi wa zamani kwa namna alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kuteka Nyoyo za mashabiki vilivyo. Kasongo mwenye asili ya Kongo aliibukia katika Hoteli ya New Afrika Dar es Salaam akiwa na MK Group, Wana NgulupaTupa Tupa na baadaye Maquiz du Zaire (Wanakamanyola) na baada ya hapo alijiunga na Wazee Sugu chini ya Mtaalamu King Kikii.


Marehemu Kasongo Mpinda Clyaton aliyeshikilia Mic enzi za uhai wake.
Kasongo alivuma sana na nyimbo zilizompandisha chati ni pamoja na 'SEYA', ANGELOU', 'MUME WANGU MWENYEWE' na "NASONONEKA" aliyeziimba kwa mtindo wa "Ogelea Piga Mbizi"

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe................R.I.P Mzee wetu Kasongo.



@RINYO'S

Maoni yako ni muhimu sana kwangu ili kuweza kujua umuhimu wangu kwako na hisia zako juu ya taarifa uliyoipata......................................
SERIKALI YA KOREA YAFUNGUA RASMI NA KUKABIDHI JENGO LA MICHEZO YA TAEKWONDO KWA JESHI LA POLISI LA TANZANIA:

Serikali ya Korea ikiwakilishwa na Balozi wake Mh. II Chung katika kuboresha mahusiano mema na Serikali ya Tanzania hiyo jana ilifanikiwa kuzindua Jengo maalumu kwa ajili ya Michezo ya Taekwondo na kulikabidhi Jeshi la Polisi lililowakilishwa na Naibu Mkuu wa Jeshi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki akiongozana na maafisa mbalimbali wa Jeshi la polisi.


Naibu Mkuu wa Jeshi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki na
Balozi wa Korea hapa nchini Mh. II Chung wakikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa jengo la kisasa la michezo ya Taekwondo ambalo lilimekabidhiwa kwa jeshi la polisi nchini.
 

Naibu Mkuu wa Jeshi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki na
Balozi wa Korea hapa nchini Mh. II Chung katika picha ya pamoja na timu ya Taekwondo baada ya makabidhiano ya Jengo hilo la kisasa tukio lililofanywa na Balozi wa Korea nchini.



Naibu Mkuu wa Jeshi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki akimkabidhi cheti Bw, Shieyoung Pyeon baada ya makabidhiano ya jengo la michezo ya Taekwondo.


@RINYO'S 

Usisahau kuweka maoni yako hapaaaa....... 
AJALI YAUA 12 HUKU DEREVA AKITOKOMEA KUSIKOJULIKANA ......(SINGIDA):

Basi la mikoani la kampuni ya TAQUIBIR limepata ajali katika kijiji cha Kisonzo Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida na kusababisha vifo vya watu 12 ambao ni wanaume saba (7) na wanawake watano (5). Basi hilo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea mji mdogo wa Katoro liligongana na lori la mafuta na kusababisha vifo hivyo vya watu 12 na kusababishia watu wengine 18 majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Singida Thobiasi Sedoyeka amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida Thobias Sedoyeka
 Akizungumzia mazingira ya ajali hiyo Kamanda alisema kuwa dereva wa Basi Bw. Charles Kaeme  alikua analipita Lori la kampuni ya Coca-Cola ndipo akagongana na Lori hilo la mafuta.

Pia Kamanda alithibitisha kutoroka kwa dereva wa basi hilo baada ya kutokea kwa ajali hiyo lakini amesema Jeshi la polisi liko kazini kumsaka dereva huyo.

Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba Timothy Sumbe amethibitisha kupokea maiti hizo 12 na kusema kuwa majeruhi 18 bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali yake.

@RINYO'S