HARMONIZE AJICHORA TATOO YA PICHA YA DIAMOND:
Picha: Harmonize achora tattoo ya picha ya boss wake Diamond na kuandika
‘Simba’
Msanii wa label ya WCB anayekuja juu kwa sasa, Harmonize ameamua
kuuthibitishia ulimwengu kuwa anajivunia kuwa mtoto wa kimuziki wa staa
wa Tanzania, Diamond Platnumz kwa kuchora tattoo yenye picha yake na
kuandika a.k.a ya Boss wake iliyozua utata hivi karibuni ‘Simba’.
Hiki ndicho alichokiandika Harmonize kwenye picha aliyoipost Instagram
kuelezea sababu za kuchora tattoo hiyo:
“Katika Maisha Yangu Sikuwahi Kuwaza Kuwa Itatokea Siku Nikajichora
Tatoo But Diamond Nimtu Mwenye Mchango Mkubwa Sanaaaa Katika Maisha
Yangu Leo Hii Mimi Ninathaminika Kutoka Kwenye Kunyanyasika
Ninaheshimika Kutoka Kwenye Kudhalaulika Nimekuwa Maarufu Na Kupata
Uthamani Mkubwa Kupitia Yeye Siotu Kwa Kipaji Nilicho Nacho Kwani
Wangapi Wanavipaji…??? Naisaidia Familia Yangu Kwa Kile Nikipatacho
Sihaba Akiwa Na Mchango Wake Mkubwa Sana…… Lakini Mwisho Wasiku Haya yote ni kwaajili ya kuonyesha kuwa nauthamini sana msaada wake wa hali na mali"
Alisema hayoHarmonize.
@RINYO'S