Saturday, 16 January 2016

JIJI LA ARUSHA LAJIPANGA KUONDOA MAKAZI HOLELA











Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya  Jiji .
Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato yanayotokana naupimaji huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi inavyotaka.
"Hatutaweza kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.
Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.


 Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro(kushoto)akiweka saini makubaliano kati ya Jiji la Arusha na kampuni ya Bondeni Seeds Limited    yatakayowezesha eneo la Heka 750 kupimwa na kuwa kwenye mpango unaoendana mpango Mji wa Jiji katika eneo la Murieti wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngarenaro,Isaya Doita,Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema,Mwanasheria wa Jiji,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd na Mwanasheria wa Bondeni Seeds Limited leo.

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akibadilishana hati za makubaliano  na Mkurugenzi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited ,Rakesh Vohora  ya kuendeleza eneo la Heka 750 eneo la Muriet linalomilikiwa na kampuni hiyo .

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza  baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo,kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro.

Diwani wa Kata ya Moshono ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji ya Jiji la Arusha,Metson Paul(kushoto) akiwa Mwanasheria  na Mkurungezi wa  kampuni ya Bondeni Seeds Limited.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo.
Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba zao.


@RINYO'S


Weka comment yako hapa.

SIASA:

UKAWA WASHINDA KITI CHA UMEYA MANISPAA YA ILALA. 

Katika Duru za Siasa tena na mara hii zinaenda kwa upande wa ucha guzi wa Meya wa Manispaa ya Ilala katika Jiji la Dar es Saalam na UKAWA wamefanikiwa kumake headlines kwa mara nyingine baada ya kuibuka washindi katika uchaguzi huo baada ya kufanikiwa kumchagua Meya wa Manispaa hiyo ambaye ni Bw. Charless Kwiyeko.  

Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya kushinda  kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto  akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  wapiga kura wakipiga kura za Meya na Naibu leo katika uchaguzi  wa kuwapata viongozi hao wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.


Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya, naibu Meya  wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kupiga kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wa UKAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mh. Freeman Mbowe wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Umeya na Unaibu Meya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakishangilia ushindi wa Meya na Naibu Meya mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi jijini Dar es Salaam leo.
 Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi wakiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee. 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na kuwashukuru madiwani leo jijini Dar es Salaam baada ya uchaguzi wa meya.
@RINYO'S

Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) yatangaza nafasi mbalimbali za kazi..........

NAFASI ZA KAZI ZILIZOPO

Kuweza kuona nafasi za kazi zilizotangazwa na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania bonyeza  hapa .


@RINYO'S

Wanasoka wa Tanzania wazidi kupata shavu Ulaya...............


 Baada ya Mbwana Sammata ambaye ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka  Afrika kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi hatimaye nyota ya kijani yazidi kuwaka kwa wanasoka mbalimbali ambao sasa wamekuwa wakihitajika Ulaya katika vilabu mbalimbali kwa ajili ya majiribio na sasa ni zamu ya winga machachari wa Azam FC Faridi Malik Mussa. 


Winga wa Azam FC Farid Mussa akiwa mazoezini.
Wanasoka wa Tanzania wamekuwa na mwamko wa kusaka fursa za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, Samatta kwenda Ubelgiji, Maguli - Misri, Farid Malilk Musa?
Winga wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Azam FC, Farid Malik Mussa anaweza kwenda Celtic FC ya Ligi Kuu ya Scotland au Athletic Bilbao ya Ligi Kuu ya Hispania kwa majaribio.
Hiyo inafuatia wakala mmoja mwenye mahusiano mazuri na klabu hizo kuwasiliana na Azam FC, inayommiliki Farid akisema Celtic na Bilbao ndizo klabu ambazo zinahitaji mchezaji aina ya Farid.
Wakala huyo amefanikiwa kuishawishi Azam FC iachane na ofa ya wakala aliyekuwa anataka kumpeleka Farid klabu ya FC Olimpija Ljubljana ya Slovenia.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Azam, wakala huyo anayetaka kumpeleka Farid Celtic au Bilbao, tayari ametuma fedha nchini ili mchezaji huyo apate kozi za masomo ya lugha ya Kiingereza.
Hata hivyo, mpango wa Slovenia ulikuwa ni wa mapema zaidi kwa Farid kwamba kama angekwenda Hispania kukutana na klabu hiyo kwa majaribio na kufuzu angesajiliwa katika dirisha hili dogo la Januari.
Lakini haijulikani mpango wa Celtic au Bilbao kama unaweza kukamilika katika dirisha hili la usajili au baadaye.
Na Mtanzania ambaye aliwaunganisha Azam FC na wakala wa timu ya Slovenia anaamini klabu hiyo imegoma kumuuza mchezaji huyo ili abaki kuwasaidia katika Ligi Kuu ya Vodacom.
Farid alitarajiwa kuondoka wiki iliyopita kwenda Hispania kuungana na klabu hiyo bingwa ya Slovenia, FC Olimpija Ljubljana iliyoweka kambi huko ambako alipewa siku 10 za majaribio.
Mabingwa hao wa Slovenia waliweka kambi nchini Hispania kujiandaa na Ligi ya kwao na Farid alitarajiwa kuwa nao kwa siku zote 10 akifanya nao mazoezi kabla ya kuamua kumnunua.

@RINYO'S