SIASA:
UKAWA WASHINDA KITI CHA UMEYA MANISPAA YA ILALA.
Katika Duru za Siasa tena na mara hii zinaenda kwa upande wa ucha guzi wa Meya wa Manispaa ya Ilala katika Jiji la Dar es Saalam na UKAWA wamefanikiwa kumake headlines kwa mara nyingine baada ya kuibuka washindi katika uchaguzi huo baada ya kufanikiwa kumchagua Meya wa Manispaa hiyo ambaye ni Bw. Charless Kwiyeko.
Meya
wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa
ya Ilala leo mara bada ya kushinda kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya
wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto akiwashukuru madiwani
waliompigia kura leo mara baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi
uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wapiga kura wakipiga kura za Meya na Naibu leo katika uchaguzi wa
kuwapata viongozi hao wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Matokeo
ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya, naibu
Meya wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kupiga kura
katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya viongozi wa UKAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mh. Freeman Mbowe wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Umeya na
Unaibu Meya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam leo.
Wananchi wakishangilia ushindi wa Meya na Naibu Meya mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi jijini Dar es Salaam leo.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi wakiteta jambo na Meya
wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko leo jijini Dar es Salaam mara
baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na kuwashukuru madiwani leo jijini Dar es Salaam baada ya uchaguzi wa meya.
@RINYO'S











No comments:
Post a Comment