Wanasoka wa Tanzania wazidi kupata shavu Ulaya...............
Baada ya Mbwana Sammata ambaye ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka Afrika kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi hatimaye nyota ya kijani yazidi kuwaka kwa wanasoka mbalimbali ambao sasa wamekuwa wakihitajika Ulaya katika vilabu mbalimbali kwa ajili ya majiribio na sasa ni zamu ya winga machachari wa Azam FC Faridi Malik Mussa.
![]() |
| Winga wa Azam FC Farid Mussa akiwa mazoezini. |
Wanasoka wa Tanzania wamekuwa na mwamko wa kusaka
fursa za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, Samatta kwenda Ubelgiji,
Maguli - Misri, Farid Malilk Musa?
Winga wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Azam FC, Farid Malik Mussa
anaweza kwenda Celtic FC ya Ligi Kuu ya Scotland au Athletic Bilbao ya
Ligi Kuu ya Hispania kwa majaribio.Hiyo inafuatia wakala mmoja mwenye mahusiano mazuri na klabu hizo kuwasiliana na Azam FC, inayommiliki Farid akisema Celtic na Bilbao ndizo klabu ambazo zinahitaji mchezaji aina ya Farid.
Wakala huyo amefanikiwa kuishawishi Azam FC iachane na ofa ya wakala aliyekuwa anataka kumpeleka Farid klabu ya FC Olimpija Ljubljana ya Slovenia.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Azam, wakala huyo anayetaka kumpeleka Farid Celtic au Bilbao, tayari ametuma fedha nchini ili mchezaji huyo apate kozi za masomo ya lugha ya Kiingereza.
Hata hivyo, mpango wa Slovenia ulikuwa ni wa mapema zaidi kwa Farid kwamba kama angekwenda Hispania kukutana na klabu hiyo kwa majaribio na kufuzu angesajiliwa katika dirisha hili dogo la Januari.
Lakini haijulikani mpango wa Celtic au Bilbao kama unaweza kukamilika katika dirisha hili la usajili au baadaye.
Na Mtanzania ambaye aliwaunganisha Azam FC na wakala wa timu ya Slovenia anaamini klabu hiyo imegoma kumuuza mchezaji huyo ili abaki kuwasaidia katika Ligi Kuu ya Vodacom.
Farid alitarajiwa kuondoka wiki iliyopita kwenda Hispania kuungana na klabu hiyo bingwa ya Slovenia, FC Olimpija Ljubljana iliyoweka kambi huko ambako alipewa siku 10 za majaribio.
Mabingwa hao wa Slovenia waliweka kambi nchini Hispania kujiandaa na Ligi ya kwao na Farid alitarajiwa kuwa nao kwa siku zote 10 akifanya nao mazoezi kabla ya kuamua kumnunua.
@RINYO'S

No comments:
Post a Comment