WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AZIDI KUUWASHA MOTO....
Huku watanzania wakiwa bado hawajaondokewa na kumbukumbu za ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa siku chache baada ya uteuzi wake katika Bandari kuu ya Dar es Salaam nakubaini upotevu wa makontena yapatayo 349, leo hii kwa mara nyingine Waziri mkuu huyo amefanya ziara nyingine ya ghafla katika Bandari hiyo pamoja na ziara nyingine katika Shirika la Reli Tanzania TRL na kuweza kugundua uozo mwingine wa upotevu wa Makontena mengine 2,431.
![]() |
| Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa |
Taarifa hii imeripotiwa na kituo cha Luninga cha ITV katika Ukurasa wao wa Tweeter.
| Sehemu ya Habari iliyotolewa na ITV katika ukurasa wao wa Tweeter kuhusu ziara nyingine ya Waziri Mkuu. |
Usisahau kutupia mawazo yako na mtazamo wako juu ya kasi ya Rais wetu mpya na Waziri Mkuu wake.......na je unaiona Tanzania wapi after 3 Years?????
@RINYO'S
