Wednesday, 2 December 2015

AJALI YAUA 12 HUKU DEREVA AKITOKOMEA KUSIKOJULIKANA ......(SINGIDA):

Basi la mikoani la kampuni ya TAQUIBIR limepata ajali katika kijiji cha Kisonzo Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida na kusababisha vifo vya watu 12 ambao ni wanaume saba (7) na wanawake watano (5). Basi hilo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea mji mdogo wa Katoro liligongana na lori la mafuta na kusababisha vifo hivyo vya watu 12 na kusababishia watu wengine 18 majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Singida Thobiasi Sedoyeka amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida Thobias Sedoyeka
 Akizungumzia mazingira ya ajali hiyo Kamanda alisema kuwa dereva wa Basi Bw. Charles Kaeme  alikua analipita Lori la kampuni ya Coca-Cola ndipo akagongana na Lori hilo la mafuta.

Pia Kamanda alithibitisha kutoroka kwa dereva wa basi hilo baada ya kutokea kwa ajali hiyo lakini amesema Jeshi la polisi liko kazini kumsaka dereva huyo.

Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba Timothy Sumbe amethibitisha kupokea maiti hizo 12 na kusema kuwa majeruhi 18 bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali yake.

@RINYO'S 

No comments:

Post a Comment