Staa wa muziki wa Bongo Fleva Ali kiba ametinga tene ndani ya South Africa kwa mara nyingine, hii
sio safari ya kwanza kwenye siku za hivi karibuni japo safari za kwanza
na hii ya sasahivi ziko tofauti kidogo..
Ali kiba ana kazi nyingine iliyomfanya akatua South Africa kwa mara nyingine.
Ali kiba yuko South Africa toka November 29 2015
akiwa kama Balozi wa kupingana na ujangili… kilichompeleka South Africa
ni ishu ya kushiriki kongamano linalowakutanisha watu mbalimbali
ikiwemo Wakurugenzi mbalimbali kutoka China na Africa pamoja na viongozi
wa taasisi za kijamii, na kati ya mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na
njia bora za kusaidia utunzaji wa wanyamapori pamoja na hifadhi.
Katika maneno ambayo Ali Kiba aliyaongea alipotoa ujumbe wake akiwa South Afrika ni pamoja na na nanukuu
“Nchi
yangu imepoteza tembo wengi sana ndani ya miaka michache iliyopita kwa
sababu ya ujangili… ni lazima tuangalie njia za kushirikiana kuhakikisha
tunazuia mauaji hayo na kulinda wanyamapori wetu.”
Pia Kiba ambaye ni staa wa ngoma ya Nagharamia alisema
“Sote
tuna majukumu kuhakikisha tunalinda wanyamapori wetu, mimi kama msanii
na mwanamuziki natumia nafasi yangu kusimamia suala hili na kuhimiza
watu wengine wengi zaidi waunge mkono hizi jitihada.”
Alikiba ni Balozi wa WildAid Campaign ambayo inapiga vita ujangili ambapo mwanzo wa November 2015 alikuwa Marekani ambako alikutana na Mabalozi wengine kama akina Fergie, Lupita Nyong’o, na mastaa wengine wakubwa Duniani… ziara hii ya Alikiba itaendelea mpaka December 03 2015 na kati ya maeneo ambayo atatembelea ni pamoja na hifadhi ya wanyama ya Kruger National Park.
@RINYO'S.


No comments:
Post a Comment