Friday, 27 November 2015

WIZARA YA MALIASILI HATIMAYE YAZUIA UHALIFU MWINGINE WA KUHUJUMU RASILIMALI ZA NCHI KUFANYIKA.

Wizara ya maliasili na utalii chini ya Katibu mkuu wa Wizara ya Dkt. Adelhelm Meru wamefanikiwa kukamata Makontena yapatayo 31 yaliyokuwa katika hatua za mwisho kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Ikumbukwe pia ni wiki chache zimepita tangu wizara hiyo kufanikiwa pia kukamata kobe 201 katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambao walikua katika hatua za mwisho kwaajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Baadhi ya Makontena yaliyokuwa yakisafirishwa kwa njia isiyohalali kama yanavyoonekana

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelm  Meru wakikagua makontena yaliyobeba magogo hayo.




@RINYO'S

No comments:

Post a Comment