Thursday, 19 November 2015

HATIMAYE TANZANIA YAFANIKIWA KUMPATA WAZIRI MKUU MPYA:

Katika siku nzima ya Ijumaa ya Tarehe 19/11/2015 habari kubwa iliyokuwa imetapakaa nchini ni habari kuhusu mchakato wa kumpata waziri mkuu wa serikali ya awamu ya ttano ambayo itakua chini ya Mh. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa awmu ya tano.

Katika kikao cha Bunge la Jamuhuri kilichoketi jina la Majaliwa Kassim Majaliwa liliwasilishwa baada ya kupendekezwa na Rais na hii ilikua ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi ambao walikuwa wakieneza tetesi huku na kule mara wakisema atakuwa huyu na wengine wakisema atakuwa yule. Majaliwa Kassim Majaliwa ambaye ni Mbunge wa Ruangwa alipigiwa na Wabunge ili kuuthibitisha uteuzi wake ambapo alifanikiwa kupitishwa kwa kishindo kwa kupata kura zaidi ya 250 ambayo ni sawa na asilimia 73% ya kura zote, na hivyo kutangazwa rasmi na Spika wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai kuwa Waziri Mkuu Mpya wa Tanzania.


Waziri Mkuu mpya wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kama anavyoonekana katika picha akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza baada ya uteuzi.
 Aidha katika hatua nyingine Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamali Malinzi amemtumia salamu za pongezi Mh. Majaliwa kupitia akaunti yake Tweeter kwa uteuzi huo kwani ni mdau mkubwa wa mpira wa miguu hapa nchi huku akiwa na Leseni ya Daraja B ya ukocha kutoka katika shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

WASIFU WA MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA:

Vijalizo vya JinaMhe.
Jina la Ukoo:Majaliwa
Jina la Kwanza:Kassim
Jina la Kati:Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa:1960-12-22
Mahali Alipozaliwa:
Hali ya Ndoa:Nimeoa
Kundi:Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Jinsia:M
Simu ya Ofisi:-
Simu ya mkononi:785205910
Barua pepe:majaliwa.kasimu@yahoo.com
Anuani:P.O.Box 51,
Ruangwa

Elimu
TokaHadiJina la Shule/ChuoCheti

19701976Mnacho Primary Schoolcheti cha Elimu ya Msingi
19771980Kigonsera Secondary SchoolCSEE
19911993Mtwara Teachers College-
19941998University of Dar es SalaamBachelor Degree
19991999Storckolm UniversityPGDP

Mafunzo Mengineyo
-

Uzoefu
TokaHadiJina la MwajiriNgazi/Nyazifa

20102014-MB
20062010PMMkuu wa Wilaya
20012006PS-CWJKatibu Mkoa
20012001PS-CWJKatibu Wilaya
19882000PS-MoecMkufunzi
19841986TD-Lindi CouncilMwalimu

@RINYO'S


No comments:

Post a Comment