Wednesday, 18 November 2015


 Wednesday 18/11/2015 (03:42 PM)

KOBE 201 WANASWA UWANJA WA KIMATAIFA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE WAKITAKA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI.

Akizungumzia tukio hilo Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru amesema kuwa kobe hao 201 walikamatwa uwanjani hapo na Askari wa Maliasili kwa ushirikiano na Askari wa usalama katika Uwanja wa ndege,wakiwa wamefungwa katika mabegi makubwa matano.



Watuhumiwa hao wa tukio hilo la usafirishaji wa Wanyamapori wametajwa kwa majina kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Tanga na Mohhamed Sulleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupenya katika mitambo ya ukaguzi katika Uwanja huo lakini Mbwa maalum (Sniffer Dogs) walisaidia kubaini uhalifu huo. Watuhumiwa hao kwa pamoja walithibitika kuwa na tiketi za kusafiria kwenda Malaysia.
























Aidha katika tukio hilo Kobe wengine 103 walikamatwa wakiwa wametelekezwa katika eneo la Tabata.

 http://elirinyouronu.blogspot.com/2015/11/18112015-0342-pm-kobe-201-wanaswa.html
 @Rinyo

No comments:

Post a Comment