Tuesday, 28 June 2016

YANGA YAKUMBANA NA KIPIGO KINGINE KUTOKA KWA TP MAZEMBE


Kiungo mshambuliaji na Nahodha wa Yanga Mnyarwanda Haruna Niyonzima akiwa kazini katika moja ya michezo ya timu zake

Licha ya kucheza katika uwanja wa nyumbani wa Taifa mbele ya mashabiki zaidi ya Elfu Arobaini (40,000) mabingwa wa soka Tanzania klabu ya Yanga ambao ndo wawakilishi pekee kwa upande wa vilabu waliosalia katika kuiwakilisha nchi jioni ya leo wameshindwa kufukuta mbele ya klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mfululizo wa michezo ya Kombe la Shirikisho la Afrika CAF.
Katika mchezo huo ambao mashabiki waliruhusiwa kuingia bure Yanga imeambulia kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Mazembe goli likifungwa na Bope.

Saturday, 7 May 2016

SOKA

MWANANDINGA WA CAMEROON APOTEZA MAISHA UWANJANI...

Baada ya kupita kwa takribani miaka 13 tangu mwanasoka mwingine nguli wa Cameroon apoteze maisha akiwa uwanjani Mark Vivian Foe usiku wa kuamkia leo yani usiku wa tarehe 06/05/2016 ulikua ni usiku mwingine wa majonzi kwa wapenzi wa soka wa Cameroon na hii ni baada ya mchezaji wao wa kimataifa anayekipiga katika klabu ya Dianamo Bucarest kupoteza maisha akiwa uwanjani.

Sunday, 24 April 2016

KUMBUKUMBU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

MIAKA MIWILI BAADA YA KIFO CHA HENRY KOGA....NA VURUGU CHUONI,


Ni takribani miaka miwili sasa imekatika baada ya Vurugu na Maandamano kuibuka katika Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA na hii ilikua ni baada ya kifo cha Mwanafunzi wa Chuo hicho Marehemu Henry Koga aliyeuawa kwa kuchomwa kisu usiku wa kuamkia tarehe 24/04/2013 alipokua akitokea maeneo ya chuo baada ya kujisomea.


Henry Koga wakati wa uhai wake.


Lilikua ni tukio lililogusa hisia za watu wengi sana hasa wanafunzi wa Chuo kizima na Asubuhi ya siku iliyofuata wanafunzi karibia wote kwa makadirio ni kama 80% ya wanafunzi wote walikusanyika kwa pamoja katika eneo la Freedom Square wakiadhimia kuandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Arusha kwa dhumuni la kujua hatma zao za Usalama wao baada ya kutokea kwa vitendo vya ukabaji wa wanafunzi na kuporwa kwa mali zao pamoja na uvamizi wa hosteli na kuibiwa mali zao na tukio la kuchomwa kisu kwa mwanafunzi mwenzao pia likawa chagizo kubwa la kutaka kujua hatma ya usalama wao.

Elirinyo huyu hapa akisimulia kile alichokishuhudia siku hiyo-

"Kiukweli mimi nilifika chuoni kama kawaida lakini sikua najua kama ishu ilikua serious kivile maana nilikuta wanafunzi weeengi wamejikusanya pamoja katika vikundivikundi wakijadili kuhusu kuandamana....ninachokumbuka ni kuwa nilifika wakati Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Kamanda Liberatus Sabasi ndiye alikua juu ghorofani akiongea na wanafunzi kwa kuwafariji lakini kuna kauli aliitoa ya kufananisha tukio hili na tukio lililotokea Zanzibar la kuuawa kwa Askofu Mushi pengine naweza kusema lile lilikua ndo kosa kwani niliwasikia wanafunzi kwa sauti za juu wakishout.....'Inahusiana na nini...Inahusiana na nini....inahusiana na nini' kelele hizi zilimfanya kamanda kushuka jukwaani, ndipo alipopanda Rais wa serikali ya Wanafunzi wawakati huo Bw, Benjamin Simkanga kuwatuliza wanafunzi kwa hekima lakini wanafunzi wakamzomea na kumwambia yuko upande wa Utawala na hataki wapate haki yao......kwa kweli hali ilikua mbaya sana na nilishaiona hali ya hatari, niliamua kuondoka eneo la tukio na kwenda kurejesha kitabu Maktaba kuepuka faini maana ilikua ndo siku ya mwisho, nilikua na matarajio ya kurejea eneo la tukio kuona nini kitaendelea lakini sikuweza kwani kuna muhudumu mmoja wa Maktaba alinishauri na kuniambia nibaki Maktaba maana hali itabadilika punde na kuwa mbaya nami nilitii ombi lake na kusalia maktaba"

-Elirinyo anatujuza nini hasa kiliendele-

"Japo nilikua Maktaba lakini kwa mbaali niliweza kuona wanafunzi wakiongozwa na Mbunge wa Arusha wakiandamana kuelekea katika ukumbi mkubwa wa Main Cafeteria huku wakiimba wimbo wa "Tunatakaaa haki zeetuu ....Tunataaaaka haki zeetu' na hii ni baada ya kuwasili kwa mkuuu wa Arusha wa wakati huo amabye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo......baada ya hapo nilikuja kujionea tuu kile kilichojiri kupitia video clip mbali mbali ambapo wanafunzi walidiriki kumfanyia fujo Mkuu wa Mkoa kwa kumrushia chupa za maji ndipo Jeshi la Polisi likaingilia kati na kumuondoa mkuu wa mkoa kwa usalama zaidi na kuanza kufyatua mabomu ya machozi....sisi tuliokuwa Maktaba hatukuweza kudhurika hata kidogo lakini waliokua nje ilikua ni mtafutano watu wakihaha huku na huko kusalimu maisha yao huku wengi wakipoteza mali zao mbalimbali ikiwemo simu, Laptops huku pia watu wa huduma za vinywaji wakipata hasara pia kutokana na vinywaji kuchukuliwa bila kulipiwa"

-Allan Zomanya alikua ni muathirika wa Mabomu ya machozi na hapa anaelezea-

"Kwa kweli mimi hapo awali nilikua silijui kabisa bomu la machozi likoje baada ya mabomu kuanza kupigwa nilikimbia na kujificha kwenye maua nyuma ya Main Cafeteria nikafanikiwa kuona kitu flani cha rangi ya silver lakini ghafla kilianzza kutoa moshi ndipo nilipoanza kuwashwa na macho nilikua nimevaa miwani na kutokana na muwasho nilichanganyikiwa na kuanza kukuna juu ya kioo cha miwani badala ya kutoa miwani ndo nijikune, kiukweli nilianza kuhisi kuishiwa nguvu ndipo nilipoamua liwalo na liwe nikaanza kukimbia kuelekea Administration nikarushiwa bomu la machozi jingine kwa mbele lakini nilibadili tu njia ila siyo kurudi....kingine nilichoshuhudia cha kusikitisha ni mdada aliyetaka kuruka mtaro kwa bahati mbaya akaishia kuanguka humo na kutupiwa bomu la machozi pale pale alipo...kwa kweli nilikimbia sana hadi Administration na kutafuta maji katika vyoo.."

Wanafunzi wengi wa Hostel walpata shida sana kwani mabomu yalikua yakirushwa katika Korido na kusambaa humo ndani...kunawanafunzi kadhaa waliokamatwa na Polisi na hii yote ilikua ni kwa ajili ya Kifo cha mwenzetu. ilikua mbaya sana wengi waliumia na kupoteza vitu vyao.

Tamko latolewa na Jeshi la Polisi tamko la kufungwa kwa chuo. Baada ya tamko hilo ulifuatia utekelezaji kwani matangazo yalibandikwa maeneo mbalimbali kama Hostel, Mbao za matangazo na Magetini ambapo tangazo lilikua likiamuru wanafunzi kutokuonekana eneo la chuo baada ya Masaa mawili huku tangazo likitolewa saa kumi kamili jioni.....ulikua ni wakati mgumu sana kwa dada zetu kwani wengine hawakua hata na Nauli na wengine kwao ni mikoa ya mbali na hawana ndugu Arusha......unataka kujua walikwenda wapi?.....

Baada ya hapo chuo kilifungwa kwa muda usiojulikana na kwa kipindi hiko tulikua tukijiandaa na Mitihani ya Final lakini ndo hivyo mambo yakabadilika, tuliweza kukaa nyumbani kwa kipindi cha mwezi mmoja mzima, tulirejea chuoni kwa barua kutoka kwa wakuu wa wilaya tunazoishi na pia kujisajilia upya Getini huku pia tukisaini fomu ya mkataba wa kutojihusisha na fujo zozote tuwapo chuoni


Tulifuatilia kujua chanzo cha kifo  cha mwenzetu lakini hadi leo hatujajua ni kipi hasa....Pumzika kwa amani Henry Koga.

MATUKIO KATIKA PICHA:


Henry Koga enzi za uhai wake

Henry Koga enzi za uhai wake

Henry Koga enzi za uhai wake

Mojawapo kati ya Post zilizosalia katika Account yake ya Facebook baada ya kifo chake

Mojawapo kati ya Post zilizosalia katika Account yake ya Facebook baada ya kifo chake

Mojawapo kati ya Post zilizosalia katika Account yake ya Facebook baada ya kifo chake
REST IN PEACE Henry Koga wanauhasibu tunakumiss....kwa kukumbushia ni kua wakati anafariki alikua ndiyo Current Mr. IAA.

@RINYO's


Sunday, 3 April 2016

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

 IAASO YATANGAZA BEI MPYA ZA STATIONARY .....NA PUNGUZO LA 50%...


Na Elirinyo Uronu

Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) kupitia kwa Waziri Mkuu wake Bw. Boniface Elibariki yatangaza rasmi kupunguza bei za Stationary Chuoni hapo. Akitoa tangazo hilo waziri mkuu wa Serikali hiyo ameeleza kuwa wamefanya hivyo ikiwa ni katika kutimiza moja kati ya ilani na ahadi walizokuwa wanazitoa wakati wa kampeni za kuomba ridhaa ya kuongoza chuoni hapo.

Bw. Boniface Elibariki ametanabaisha kwamba hatua hiyo itawawezesha wanafunzi kuweza kumudu gharama za maisha chuoni hapo ikiwa ni pamoja na gharama hizo za Stationary.

katika taarifa hiyo inaonyesha kuwa Bei za Kuchapa (Printing) zimeshuka kwa asilimia takribani 50% kutoka Tsh. 200/= hadi Tsh. 100/= kwa ukurasa huku gharama za kutoa nakala (Photocopying) zikishuka pia kwa assilimia 50% kutoka Tsh. 50/= kwa kurasa hadi Tsh. 25/=

Tangazo la bei mpya za Uchapaji na kutoa Nakala kama linavyoonekana

@RINYO's 

Sunday, 20 March 2016

SIASA:

CCM HIVI LEO YATANGAZA MSEMAJI WAKE MPYA:

Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho Ndugu Nape Nnauye ambapo kwa sasa Olesendeka pichani kati ndiye ameishika nafasi hiyo.

Chama cha Mapinduzi CCM leo kimemtangaza Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji mpya wa CCM kuanzia leo.Sendeka ametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam 


Msemaji mpya wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Christopher Ole Sendeka akiongea baada ya kuteuliwa siku ya leo. kulia ni aliyekua katibu mkuu mwenezi Ndugu Nape Nauye.

 @RINYO'S

Wednesday, 17 February 2016

UDAKU:

Wema Sepetu kathibitisha ujauzito wake kuharibika…


Hii ni post aliyoiandika Mwigizaji Wema Sepetu saa kadhaa baada ya Baba Watoto mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan kuthibitisha kwamba ujauzito huo wa mapacha umeharibika.
Ni kweli, na imeniuma sana lakini kwenye hatua maishani mwangu naweza kusema Alhamdulillah kwa kila kitu, Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilio nao na wameonyesha moyo wa kibinadamu, nawashukuru kwa upendo wenu.. MNANIPA NGUVU.
wema
Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wamefurahia kwasababu zao binafsi. Nawashukuru kwa uwepo wenu, MNANIPA UJASIRI, Alhamdulillah kwa siku ya kesho Ilimradi nina pumzi, SITACHOKA KUJARIBU TENA.

Wema 2Hata ukikosa, ukakosa, ukokosa eeeeeeh…sema ASANTE, KWELI YEYE NI MUNGU…. alimalizia kuandika Wema Sepetu….

 ##Millardayo

@RINYO'S 

Tuesday, 16 February 2016

MAKALA MAALUM YA FRESHERS:

CERTIFICATES WAIBUKA MABINGWA MBELE YA BARCHELOR  ONE:


Kikosi cha Certificate kilichofanikiwa kuibuka Mabingwa wa Freshers Cup kwa msimu wa 2015/2016 katika picha ya pamoja kabla ya mechi (Picha na Fransis Steven)


Kikosi cha Barchelor one kilichocheza mchezo wa Fainali ya  Freshers Cup kwa msimu wa 2015/2016 katika picha ya pamoja kabla ya mechi (Picha na Fransis Steven)

Kwa mara ya kwanza kabisa katika chuo cha Uhasibu Arusha katika mashindano ya kuwakaribisha wanafunzi wote wa Mwaka wa kwanza alimaarufu kwa Jina la Freshers Cup kuwakutanisha washindani wawili katika fainali ambao wote ni Wa mwaka wa kwanza au "Fresh", katika mashindano hayo yaliyohusisha timu sita yalishuhudia Timu ya Certificate ikifuzu kutinga hatua ya Fainali kukumbana na timu ya Barchelor One.

Mashindano hayo yalianzia hatua ya Makundi ambapo makundi yalikua kama ifuatavyo.




        KUNDI A:                                                      
1. Diploma One                                            
2. Diploma Two                                            
3. Certificate                                                 


     KUNDI B: 
1. Barchelor One
2. Barchelor Two 
3. Barchelor Three 

Misimamo katika makundi yote ilikua kama ifuatavyo

  
KUNDI A:
                               P   W   D     L   GS  GA  GD  Pts          
1. Certificate          2    1     1     0     1     0    +1      4 
2. Diploma Two     2    1     0     1     1     1      0      3
3. Diploma One     2    0     1     1     0     1     -1      1


KUNDI B:
                                 P   W   D     L   GS  GA  GD  Pts          
1. Barchelor One      2    1     1     0    3     1     +2     4 
2. Barchelor Three   2    1     0     1     1     2     -1      3
3. Barchelor Two     2    0     1     1     1     2     -1      1


Baada ya misimamo kuwa hivyo katika hatua ya makundi timu nne ziliingia hatua ya Nusu Fainali ambapo Mshindi kutoka kundi A alikabiliana na Mshindi wa pili wa kundi B (Certificate Vs Barchelor Three) nusu fainali ya pili ilikua ni kati ya Mshindi wa kwanza wa kundi B dhidi ya mshindi wa pili wa kundi A (Barchelor One Vs Diploma Two)

Katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza tulishuhudia mpira ukiisha dakika 90 timu zikiwa zimefungana 1 - 1, hivyo kuamriwa kupigwa kwa penalti ili tuweze kujua ni timu ipi itatinga fainali.
katika penalti hizo Barchelor Three walikosa Penalti 3 na kupata mbili tu huku Certificate wakiibuka kwa kupata Penalti 3 na kukosa 2, na hivyo Certificates kutinga hatua ya Fainali.

Katika Nusu Fainali ya pili ambapo kulikua na rapsha za hapa na pale kati ya Barchelor One Vs Diploma Two ambapo katika mchezo huo Barchelor One  waliibuka washindi kwa goli 1 - 0
Katika mchezo huo tuliweza kushuhudia kadi Nyekundu mbili zikitoka kwa Mchezaji wa Diploma Two Steven na nyingine ikitoka kwa Mshambuliaji wa Barchelor One Hadji Alawi baada ya kuleteana vurugu za hapa na pale ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kurushiana makonde. Pia tuliweza kushuhudia Hadji Alawi akiwahishwa hospitali baada ya kupigwa katika eneo la mshipa na steven na hivyo kuwa katika hali mbaya kama hilo halitoshi pia magolikipa wa timu zote mbili kwa nyakati tofauti tofauti waliweza kuonyeshwa kadi za njano.

Barchelor One walimpoteza pia mchezaji wao muhimu wa safu ya ulinzi Ackley ambaye alipata majeraha katika mguu wake baada ya kukabiliana na mchezaji wa Diploma Two Muze.

FAINALI:

Siku ya Jumamosi ndiyo ilikua siku ya fainali ambayo ilitanguliwa na michezo kadha wa kadha ya utangulizi ikiwemo Riadha Mbio ndefu (Mita 300) na mbio fupi (Mita 100), kukimbiza kuku, kukimbia na Magunia, kuvuta kamba na Special Ladies Match.

Katika Mashindano ya Riadha Mbio ndefu (Mita 300) na Fupi (Mita 100)
Kwa wanaume Steven aliibuka mshindi na kujinyakulia Tsh. 40,000/= huku kwa upande wa wasichana mshindi aliibuka Jackline na kujipatia pia Tsh. 40,000/=

Katika mashindano ya kukimbia na magunia Mathew Ndagile aliibuka mshindi wa pili.

Katika shindano la kukimbiza kuku Kajanja aliweza kujichukulia kuku na wengine pia.

Katika shindano la kuvuta kamba Timu Machuma chuma iliibuka kidedea na kuzawadiwa Kreti moja la Soda.

Katika mechi maalumu ya wasichana iliyowakutanisha Barchelors Ladies na Diploma + Certificate Ladies Barchelor waliibuka washindi kwa kushinda goli 1 - 0, goli lililofungwa na mshambuliaji wao hatari aitwaye Asia. Mgeni Rasmi katika pambano hilo alikua ni Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo ambaye aliongeza zawadi kwenye Mechi ya Ladies na kufanya wote wajipatie zawadi ya Kreti tatu kila timu.

Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo akisalimiana na Nahodha wa Combine ya Ladies wa Diploma na Certificate Nazve katika mpambano maalumu wa timu za wadada (Picha na Francis Steven)
Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji wa timu ya wadada ya Barchelor "Josephine" katika mpambano maalumu wa timu za wadada (Picha na Francis Steven)
Katika Mpambano husika, Mkuu wa chuo pia ndo alikua mgeni Rasmi, katika pambano hili lilishuhudia Barchelor One wakiongoza kwa Goli moja Goli lililowekwa kambani na mshambuliaji wao Gwasa mnamo dakika ya 28. 
Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo, Afisa mikopo Benjamin Semkanga na viongozi wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo Cha Uhasibu Arusha wakiongozwa na Rais wa IAASO Regnal Massawe wakiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Barchelor One kabla ya mpambano wa Fainali.  (Picha na Francis Steven)
Waamuzi waliochezesha mpambano wa Fainali kati ya Barchelor One Vs Certificate (Abeli Kipunje - Mwaamuzi wa kati, Erick Dominick - Line One na Chikito Bashoni - Line Two) wakiwa katika picha ya pamoja na Mrusha matangazo wa mpambano wa Fainali Elirinyo Uronu (Picha na Francis Steven).
Lakini kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku Certificate wakitaka kusawazisha goli na Barchelor wakilinda goli lao na kusaka goli lingine. 

Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo akisalimiana na Mshambuliaji wa Certificate Shaabani kabla ya kuanza kwa pambano la fainali  ya Freshers Cup (Picha na Francis Steven)

Juhudi za Certificate zilizaa matunda mnamo dakika ya 56 ambapo mshambuliaji wao Westron aliweza kuisawazishia timu yake goli baada ya uzembe uliofanywa na mabeki wa Barchelor kuondosha Krosi iliyopigwa na Shabani katika eneo lao la hatari, kama hiyo haitoshi huku bado Barchelor wakiendelea kutafakari mnamo dakika ya 61 Mshambuliaji wa Certificate Shabani ambaye alikua akiinyanyasa safu ya ulinzi ya Barchelor kama anavyotaka aliweza kuwainua mashabiki wa Certificate kwa mara ya pili baada ya kuiandikia goli la pili.

Wachezaji wa Barchelor One walijipanga tena na kuanza kucheza kwa kasi kutaka kukomboa goli, huku watu wengi wakiamini Barchelor wamelala kwa goli 2 - 1 mnamo dakika ya 86 mchezaji wao msumbufu Sajan aliweza kuisawazishia timu yake goli baada ya kupiga kichwa kilichodundadunda kabla ya kutinga kimiani.

Baada ya hapo timu ya Certificate walianza kupoteana lakini hadi mwamuzi anamaliza mpira dakika ya 90 matokeo yalikua ni Certifiacate 2 - 2 Barchelor One.

Mwamuzi akaamuru mshindi apatikane kwa Penalti ambapo timu zilifikia hadi kupiga Penalti 10. katika penalti 5 Tano za awali kila timu ilikosa penalti 3 na kupata penalti 2. Katika hatua hiyo ya Pennalti makipa wa timu zote mbili walionekana kufanya kazi ya ziada kuzipatia timu zao ushindi lakini aliyeibuka shujaa ni Golikipa wa Certifacate Yohana ambaye aliweza kuipangua penalti ya mwisho ya Barchelor One na kufanya timu yake iweze kutangazwa kuwa Mabingwa wapya wa Freshers Cup kwa mwaka 2016.

Vikosi vya timu zote mbili vilikua kama ifuatavyo.

CERTIFICATE:                               BARCHELOR ONE:
1. Yohana                                         1. Issa Kasekulo
2. Kubalah                                       2. Ally
3. Hasheem                                      3. Yaccoub
4. Muna                                           4. Mwakatobe Fred
5. John                                             5. Dullah (C)
6. Mliga                                           6. Ambrose
7. Shabani                                        7. Eddy
8. Pinto                                            8. Ashton
9. Weston                                         9. Gwassa
10. Athumani                                  10. Hamad
11. Gabriel                                      11. Sajo

TAKWIMU:

- Hadi mashindano yanafikia ukingoni takwimu zilikua kama ifuatavyo.
- Magoli yaliyofungwa kwa ujumla 14
- Mechi iliyoshuhudia magoli mengi ni mchezo wa Fainali ukishuhudia magoli 4 (2 - 2)
- Jumla ya kadi nyekundu 4 (Mbili katika mchezo wa Nusu Fainali ya Pili).
- Jumla ya kadi za Njano ni 19
- Mechi iliyohudhuriwa na mashabiki wengi zaidi ni mechi ya Fainali
- Mechi iliyochezwa kwa muda mrefu zaidi ni mchezo wa fainali baada ya hatua ya Penalti.





Makala maalumu ya Freshers Cup prepared by Elirinyo Uronu.



@RINYO'S



Thursday, 11 February 2016

KITAIFA:

KIVUKO CHA MAGOGONI CHAZUA TAHARUKI KUU KWA ABIRIA.......


Taarifa zilizozagaa na kushtua Umma wa Watanzania  ni pamoja na hii ya Pantoni kuzima ghafla Dar na kulazimika abiria wajitose baharini kuokoa maisha yao, hadi sasa haijafahamika kama kuna athari iliyopatikana. Nitaendelea kukujuza kadri nitakavyozidi kupata taarifa, hiyo ni ahadi yangu kwako.






3
Abiria wa kivuko cha Magogoni kama wanavyoonekana wakijitahidi kuokoa maisha yao baada ya kivuko hicho kupoteza muelekeo na kuanza kuingiza maji ndani.
.
IMG-20160211-WA0012
Abiria wa kivuko cha Magogoni kama wanavyoonekana wakijitahidi kuokoa maisha yao baada ya kivuko hicho kupoteza muelekeo na kuanza kuingiza maji ndani.
IMG-20160211-WA0009
Abiria wa kivuko cha Magogoni kama wanavyoonekana wakijitahidi kuokoa maisha yao baada ya kivuko hicho kupoteza muelekeo na kuanza kuingiza maji ndani.





@RINYO'S

BURUDANI:



HARMONIZE AJICHORA TATOO YA PICHA YA DIAMOND:



Picha: Harmonize achora tattoo ya picha ya boss wake Diamond na kuandika ‘Simba’ 


Msanii wa label ya WCB anayekuja juu kwa sasa, Harmonize ameamua kuuthibitishia ulimwengu kuwa anajivunia kuwa mtoto wa kimuziki wa staa wa Tanzania, Diamond Platnumz kwa kuchora tattoo yenye picha yake na kuandika a.k.a ya Boss wake iliyozua utata hivi karibuni ‘Simba’. Hiki ndicho alichokiandika Harmonize kwenye picha aliyoipost Instagram kuelezea sababu za kuchora tattoo hiyo: 

“Katika Maisha Yangu Sikuwahi Kuwaza Kuwa Itatokea Siku Nikajichora Tatoo But Diamond Nimtu Mwenye Mchango Mkubwa Sanaaaa Katika Maisha Yangu Leo Hii Mimi Ninathaminika Kutoka Kwenye Kunyanyasika Ninaheshimika Kutoka Kwenye Kudhalaulika Nimekuwa Maarufu Na Kupata Uthamani Mkubwa Kupitia Yeye Siotu Kwa Kipaji Nilicho Nacho Kwani Wangapi Wanavipaji…??? Naisaidia Familia Yangu Kwa Kile Nikipatacho Sihaba Akiwa Na Mchango Wake Mkubwa Sana…… Lakini Mwisho Wasiku Haya yote ni kwaajili ya kuonyesha kuwa nauthamini sana msaada wake wa hali na mali"

Alisema hayoHarmonize.


@RINYO'S

RINYO'S: ZIARA YA WAZIRI MKUU YA KUSHTUKIZA:

RINYO'S: ZIARA YA WAZIRI MKUU YA KUSHTUKIZA:: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO Waziri mkuu wa jamhuri ya M...

Sunday, 31 January 2016

ZIARA YA WAZIRI MKUU YA KUSHTUKIZA:

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.




Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  picha za mionzi (X Ray) katika hospitali  ya rufaa  ya Mawenzi.
Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa  Mwako.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo , Mhe. James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi.                                       

KITAIFA.

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA LEO IKULU DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Dkt. 
Mahadhi Juma Maalim baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo baada ya kumuapisha  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve bvaada ya kumuapisha  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kabla ya  kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Kamishna wa Polisi  Paul Amani Moses Chagonja baada ya kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 
 
 
@RINYO'S