![]() |
| Kiungo mshambuliaji na Nahodha wa Yanga Mnyarwanda Haruna Niyonzima akiwa kazini katika moja ya michezo ya timu zake |
Licha ya kucheza katika uwanja wa nyumbani wa Taifa mbele ya mashabiki zaidi ya Elfu Arobaini (40,000) mabingwa wa soka Tanzania klabu ya Yanga ambao ndo wawakilishi pekee kwa upande wa vilabu waliosalia katika kuiwakilisha nchi jioni ya leo wameshindwa kufukuta mbele ya klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mfululizo wa michezo ya Kombe la Shirikisho la Afrika CAF.
Katika mchezo huo ambao mashabiki waliruhusiwa kuingia bure Yanga imeambulia kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Mazembe goli likifungwa na Bope.

No comments:
Post a Comment