Tuesday, 16 February 2016

MAKALA MAALUM YA FRESHERS:

CERTIFICATES WAIBUKA MABINGWA MBELE YA BARCHELOR  ONE:


Kikosi cha Certificate kilichofanikiwa kuibuka Mabingwa wa Freshers Cup kwa msimu wa 2015/2016 katika picha ya pamoja kabla ya mechi (Picha na Fransis Steven)


Kikosi cha Barchelor one kilichocheza mchezo wa Fainali ya  Freshers Cup kwa msimu wa 2015/2016 katika picha ya pamoja kabla ya mechi (Picha na Fransis Steven)

Kwa mara ya kwanza kabisa katika chuo cha Uhasibu Arusha katika mashindano ya kuwakaribisha wanafunzi wote wa Mwaka wa kwanza alimaarufu kwa Jina la Freshers Cup kuwakutanisha washindani wawili katika fainali ambao wote ni Wa mwaka wa kwanza au "Fresh", katika mashindano hayo yaliyohusisha timu sita yalishuhudia Timu ya Certificate ikifuzu kutinga hatua ya Fainali kukumbana na timu ya Barchelor One.

Mashindano hayo yalianzia hatua ya Makundi ambapo makundi yalikua kama ifuatavyo.




        KUNDI A:                                                      
1. Diploma One                                            
2. Diploma Two                                            
3. Certificate                                                 


     KUNDI B: 
1. Barchelor One
2. Barchelor Two 
3. Barchelor Three 

Misimamo katika makundi yote ilikua kama ifuatavyo

  
KUNDI A:
                               P   W   D     L   GS  GA  GD  Pts          
1. Certificate          2    1     1     0     1     0    +1      4 
2. Diploma Two     2    1     0     1     1     1      0      3
3. Diploma One     2    0     1     1     0     1     -1      1


KUNDI B:
                                 P   W   D     L   GS  GA  GD  Pts          
1. Barchelor One      2    1     1     0    3     1     +2     4 
2. Barchelor Three   2    1     0     1     1     2     -1      3
3. Barchelor Two     2    0     1     1     1     2     -1      1


Baada ya misimamo kuwa hivyo katika hatua ya makundi timu nne ziliingia hatua ya Nusu Fainali ambapo Mshindi kutoka kundi A alikabiliana na Mshindi wa pili wa kundi B (Certificate Vs Barchelor Three) nusu fainali ya pili ilikua ni kati ya Mshindi wa kwanza wa kundi B dhidi ya mshindi wa pili wa kundi A (Barchelor One Vs Diploma Two)

Katika mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza tulishuhudia mpira ukiisha dakika 90 timu zikiwa zimefungana 1 - 1, hivyo kuamriwa kupigwa kwa penalti ili tuweze kujua ni timu ipi itatinga fainali.
katika penalti hizo Barchelor Three walikosa Penalti 3 na kupata mbili tu huku Certificate wakiibuka kwa kupata Penalti 3 na kukosa 2, na hivyo Certificates kutinga hatua ya Fainali.

Katika Nusu Fainali ya pili ambapo kulikua na rapsha za hapa na pale kati ya Barchelor One Vs Diploma Two ambapo katika mchezo huo Barchelor One  waliibuka washindi kwa goli 1 - 0
Katika mchezo huo tuliweza kushuhudia kadi Nyekundu mbili zikitoka kwa Mchezaji wa Diploma Two Steven na nyingine ikitoka kwa Mshambuliaji wa Barchelor One Hadji Alawi baada ya kuleteana vurugu za hapa na pale ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kurushiana makonde. Pia tuliweza kushuhudia Hadji Alawi akiwahishwa hospitali baada ya kupigwa katika eneo la mshipa na steven na hivyo kuwa katika hali mbaya kama hilo halitoshi pia magolikipa wa timu zote mbili kwa nyakati tofauti tofauti waliweza kuonyeshwa kadi za njano.

Barchelor One walimpoteza pia mchezaji wao muhimu wa safu ya ulinzi Ackley ambaye alipata majeraha katika mguu wake baada ya kukabiliana na mchezaji wa Diploma Two Muze.

FAINALI:

Siku ya Jumamosi ndiyo ilikua siku ya fainali ambayo ilitanguliwa na michezo kadha wa kadha ya utangulizi ikiwemo Riadha Mbio ndefu (Mita 300) na mbio fupi (Mita 100), kukimbiza kuku, kukimbia na Magunia, kuvuta kamba na Special Ladies Match.

Katika Mashindano ya Riadha Mbio ndefu (Mita 300) na Fupi (Mita 100)
Kwa wanaume Steven aliibuka mshindi na kujinyakulia Tsh. 40,000/= huku kwa upande wa wasichana mshindi aliibuka Jackline na kujipatia pia Tsh. 40,000/=

Katika mashindano ya kukimbia na magunia Mathew Ndagile aliibuka mshindi wa pili.

Katika shindano la kukimbiza kuku Kajanja aliweza kujichukulia kuku na wengine pia.

Katika shindano la kuvuta kamba Timu Machuma chuma iliibuka kidedea na kuzawadiwa Kreti moja la Soda.

Katika mechi maalumu ya wasichana iliyowakutanisha Barchelors Ladies na Diploma + Certificate Ladies Barchelor waliibuka washindi kwa kushinda goli 1 - 0, goli lililofungwa na mshambuliaji wao hatari aitwaye Asia. Mgeni Rasmi katika pambano hilo alikua ni Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Johannes Monyo ambaye aliongeza zawadi kwenye Mechi ya Ladies na kufanya wote wajipatie zawadi ya Kreti tatu kila timu.

Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo akisalimiana na Nahodha wa Combine ya Ladies wa Diploma na Certificate Nazve katika mpambano maalumu wa timu za wadada (Picha na Francis Steven)
Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji wa timu ya wadada ya Barchelor "Josephine" katika mpambano maalumu wa timu za wadada (Picha na Francis Steven)
Katika Mpambano husika, Mkuu wa chuo pia ndo alikua mgeni Rasmi, katika pambano hili lilishuhudia Barchelor One wakiongoza kwa Goli moja Goli lililowekwa kambani na mshambuliaji wao Gwasa mnamo dakika ya 28. 
Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo, Afisa mikopo Benjamin Semkanga na viongozi wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo Cha Uhasibu Arusha wakiongozwa na Rais wa IAASO Regnal Massawe wakiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Barchelor One kabla ya mpambano wa Fainali.  (Picha na Francis Steven)
Waamuzi waliochezesha mpambano wa Fainali kati ya Barchelor One Vs Certificate (Abeli Kipunje - Mwaamuzi wa kati, Erick Dominick - Line One na Chikito Bashoni - Line Two) wakiwa katika picha ya pamoja na Mrusha matangazo wa mpambano wa Fainali Elirinyo Uronu (Picha na Francis Steven).
Lakini kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku Certificate wakitaka kusawazisha goli na Barchelor wakilinda goli lao na kusaka goli lingine. 

Mgeni Rasmi wa Fainali ya Freshers Cup Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Professor Johhaness Monyo akisalimiana na Mshambuliaji wa Certificate Shaabani kabla ya kuanza kwa pambano la fainali  ya Freshers Cup (Picha na Francis Steven)

Juhudi za Certificate zilizaa matunda mnamo dakika ya 56 ambapo mshambuliaji wao Westron aliweza kuisawazishia timu yake goli baada ya uzembe uliofanywa na mabeki wa Barchelor kuondosha Krosi iliyopigwa na Shabani katika eneo lao la hatari, kama hiyo haitoshi huku bado Barchelor wakiendelea kutafakari mnamo dakika ya 61 Mshambuliaji wa Certificate Shabani ambaye alikua akiinyanyasa safu ya ulinzi ya Barchelor kama anavyotaka aliweza kuwainua mashabiki wa Certificate kwa mara ya pili baada ya kuiandikia goli la pili.

Wachezaji wa Barchelor One walijipanga tena na kuanza kucheza kwa kasi kutaka kukomboa goli, huku watu wengi wakiamini Barchelor wamelala kwa goli 2 - 1 mnamo dakika ya 86 mchezaji wao msumbufu Sajan aliweza kuisawazishia timu yake goli baada ya kupiga kichwa kilichodundadunda kabla ya kutinga kimiani.

Baada ya hapo timu ya Certificate walianza kupoteana lakini hadi mwamuzi anamaliza mpira dakika ya 90 matokeo yalikua ni Certifiacate 2 - 2 Barchelor One.

Mwamuzi akaamuru mshindi apatikane kwa Penalti ambapo timu zilifikia hadi kupiga Penalti 10. katika penalti 5 Tano za awali kila timu ilikosa penalti 3 na kupata penalti 2. Katika hatua hiyo ya Pennalti makipa wa timu zote mbili walionekana kufanya kazi ya ziada kuzipatia timu zao ushindi lakini aliyeibuka shujaa ni Golikipa wa Certifacate Yohana ambaye aliweza kuipangua penalti ya mwisho ya Barchelor One na kufanya timu yake iweze kutangazwa kuwa Mabingwa wapya wa Freshers Cup kwa mwaka 2016.

Vikosi vya timu zote mbili vilikua kama ifuatavyo.

CERTIFICATE:                               BARCHELOR ONE:
1. Yohana                                         1. Issa Kasekulo
2. Kubalah                                       2. Ally
3. Hasheem                                      3. Yaccoub
4. Muna                                           4. Mwakatobe Fred
5. John                                             5. Dullah (C)
6. Mliga                                           6. Ambrose
7. Shabani                                        7. Eddy
8. Pinto                                            8. Ashton
9. Weston                                         9. Gwassa
10. Athumani                                  10. Hamad
11. Gabriel                                      11. Sajo

TAKWIMU:

- Hadi mashindano yanafikia ukingoni takwimu zilikua kama ifuatavyo.
- Magoli yaliyofungwa kwa ujumla 14
- Mechi iliyoshuhudia magoli mengi ni mchezo wa Fainali ukishuhudia magoli 4 (2 - 2)
- Jumla ya kadi nyekundu 4 (Mbili katika mchezo wa Nusu Fainali ya Pili).
- Jumla ya kadi za Njano ni 19
- Mechi iliyohudhuriwa na mashabiki wengi zaidi ni mechi ya Fainali
- Mechi iliyochezwa kwa muda mrefu zaidi ni mchezo wa fainali baada ya hatua ya Penalti.





Makala maalumu ya Freshers Cup prepared by Elirinyo Uronu.



@RINYO'S



No comments:

Post a Comment