Saturday, 26 December 2015

Arsenal yazidi kuisogelea Leceister City kileleni..........Ozil azidi kungara EPL...........!!

Ikitumia vyema Uwanja wake wa nyumbani wa Emirates usiku wa Tarehe 21/12/2015 katika mwendelezo wa Ligi kuu nchini Uingereza timu ya Arsenal maarufu kama The Gunners imeweza kuifunga timu ya Manchester City kwa jumla ya magoli 2-1 na hivyo kuzidi kuipumulia klabu ya Leceister City ambao ndio vinara wa ligi.


Theo Walcott akishangilia na Mesut Ozil baada ya kuipatia Arsenal goli la kwanza
 Mpambano ulianza kwa kasi huku kila timu ikichukua tahadhari ya kutokupoteza mchezo huo, lakini mnamo dakika ya 33 ya mchezo mshambuliaji Theo Walcot aliipatia Arsenal goli la kuongoza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mesut Ozil "Pass Master".
Wachezaji wa Arsenal wakipongezana baada ya kujipatia goli la kuongoza.

3290
Mvuto wa mchezo huu unakuja kutokana na timu zote kuwa katika nafasi tatu za juu, hivyo ushindi kwa kila timu ulikuwa ni muhimu kwani utakuwa unamuweka karibu na Leicester City inayoongoza. Kama hiyo haitoshi mnamo dakika ya 45 ya mchezo Olivier Girou alipokea pasi kutoka kwa Ozil tena na kuifungia Arsena goli la pili.
Hadi mpira unakwenda mapumziko ubao ulisomeka Arsenal 2-1 Manchester City.

3157
Mshambuliaji Olivier Giroud akiifungia Arsenal goli la pili.

4779
Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake wa kifaransa Oliver Giroud alipachika wavuni goli la pili dakika ya 45 na kuufanya mchezo kumalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Man City, huku goli la Man City likifungwa na Yaya Toure dakika ya 82. Kwa matokeo hayo Arsenal wanakuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi wakiwa na jumla ya point 36 tofauti ya point 2 na Leicester City wanaoongoza Ligi.
4238

Monday, 14 December 2015

CURTHBET MASSAWE AZIKWA LEO HUKO  MASAMA MKOANI KILIMANJARO.

Leo ilikua ni siku nyingine ya majonzi kwa Chuo cha Uhasibu Arusha kutokana na mazishi ya kijana wao mpendwa wa Shahada ya Uhasibu  mwaka wa pili marehemu Curthbet Massawe, Marehemu alifariki katika ajali iliyohusisha pia kupoteza uhai wa kijana mwingine wa Uhasibu Marehemu Emmanuel Sabuni ambaye yeye alipumzishwa rasmi katika nyumba yake ya milele siku ya Jumamosi ya tarehe 12/12/2015.

Katika mazishi hayo yaliyoonekana kugusa watu wengi Chuo cha Uhasibu kikiongozwa na Mwadili wa wanafunzi (Matron) kilitoa jumla ya waombolezaji zaidi ya 350 ili kuwawakilisha wanafunzi wote katika kuifariji familia ya marehemu Curthbert Massawe.


Mazishi haya yalisababisha watu wengi kutokwa na machozi na wengine hata kupoteza fahamu hasa ukizingatia kuwa kijana alikua bado ni mdogo mno kwani amefariki akiwa na umri wa miaka 26 tu.

Mwili wa marehemu uliagwa rasmi katika Vyumba vya kuhifadhia maiti (Mouchwary) katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru majira ya saa tatu, na ndipo safari ya kuelekea Moshi ilipoanza ikijumuisha Coster 8 zilizobeba wanafunzi na magari mengine ya watu binafsi yapatayo 6, kabla ya safari kuanza ilifanyika sala ya kumuombea marehemu na pia kuibariki safari, pia baba na mama wa Marehemu Emmanuel Sabuni ambaye walipata ajali pamoja na Curthbet alitoa neno la faraja kwa wazazi wa Curthbet pamoja na kwa waombolezaji kisha akatutakia safari njema.


Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Tema akiweka shada pamoja na mchungaji mwenzake katika kaburi la Curthbet Massawe. (Picha na Elirinyo).

Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Tema akiweka shada pamoja na mchungaji mwenzake katika kaburi la Curthbet Massawe. (Picha na Elirinyo).
Baba na Mama (Wazazi) wa Curthbet wakiweka shada katika kaburi la mwanao.(Picha na Elirinyo)

Baba na Mama (Wazazi) wa Curthbet wakiweka shada katika kaburi la mwanao.(Picha na Elirinyo)



Mwadili wa wanafunzi (Matron) katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) akiweka shada kwa niaba ya Management.(Picha na Elirinyo)



Kaka zake na Curthbet wakiweka mashada katika kaburi la mdogo wao (Picha na Elirinyo)

Mjomba akienda kuweka shada katika kaburi la marehemu (Picha na Elirinyo).


Mama wadogo wa Marehemu wakiweka mashada yao (Picha na Elirinyo)


 Marehemu Curthbet atakumbukwa kwa mengi sana, katika shule yake ya Sekondari ya Nkokashu alitumika kama Mwenyekiti wa UKWATA ambapo alisoma hapo tangu mwaka 2004-2007 vivyo hivyo akiwa katika chuo cha Uhasibu (IAA) aimtumikia Mungu kwa namna ya tofauti kwani alikua ni mpiga vyombo kama Drums na Kinanda. Hakika Mungu amechukua kile kilicho chake.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.  Amen!!

@RINYO'S


Sunday, 13 December 2015

UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI WAFANYIKA LEO:


Uchaguzi huu ambao ulihairishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa chama cha ACT Wazalendo Bw. Estomihi Mala umekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwitikio kuwa mdogo, pia mvua za hapa na pale. Sababu za mwitikio kuwa mdogo watu wengi wamelalamikia vitendo vya kubakwa kwa demokrasia kutokana na wao kuchagua kiongozi wanayempenda lakini badala ya kupewa waliomchagua wanapewa kiongozi wakuchaguliwa, pia wengine wanadai ni kutokana na sherehe zinazoendelea ikiwa ni pamoja na sherehe za Kipaimara.

Habari zaidi zitakujia...............................


@RINYO'S

Saturday, 12 December 2015

MATUKIO:

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAFANIKIWA KUMZIKA EMMANUEL SABUNI SALAMA.

Leo katika eneo la Njiro kulikua na mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Marehemu Emmanuel Robson Sabuni ambaye alipoteza maisha siku ya Jumatano ya Tarehe 09/12/2015 kutokana na ajali iliyohusisha gari aina ya Land Cruiser na pikipiki waliyokua wakiitumia kusafiria kuelekea mjini ambapo katika ajali hiyo Emmanuel alikua pamoja na mwanafunzi mwenzake aitwaye Carthbet Massawe ambaye naye pia alipoteza maisha kutokana na ajali hiyo. 

Emmanuel amefariki akiwa na umri wa miaka 25 tu, ambapo alizaliwa mnamo Tarehe 25/05/1990 na kufariki Tarehe 09/12/2015 siku ya Jumatano. 

Baadhi ya waombolezaji wakiondoka nyumbani kwa mzee Robison Sabuni baba mzazi wa marehemu eneo la Kikokwaru (Double B) kuelekea kanisani ilipofanyika ibada ya maziko. (Picha na Elirinyo).

Baadhi ya waombolezaji wakiondoka nyumbani kwa mzee Robison Sabuni baba mzazi wa marehemu eneo la Kikokwaru (Double B) kuelekea kanisani ilipofanyika ibada ya maziko. (Picha na Elirinyo).

Ibada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ambapo Ibada iliongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika Mch. Letare, ambaye katika mahubiri yake aliwakumbusha wote waliohudhuria safari hiyo ya mwisho ya mpendwa wetu Emmanuel kujiweka tayari kwa ni kwani ni kwa wakati wowote tena tusiodhani tunaweza kukumbwa na mauti kwani kifo kimeumbiwa mwanadamu, Mch. Letare akitumia neno kutoka kitabu cha nabii Isaya 37:1-8 alisema ni wakati wa sisi kujikita katika kutenda mema ili hata wakati wa hukumu yetu tupate kumkumbusha Mungu kwa yale mema tuliyokwisha kuyafanya kama alivyofanya Mfalme Hezekia.


Lango kuu la kuingilia Kanisa la KKKT usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ilipofanyikia ibada ya mazishi ya Emmanueli Sabuni. (Picha na Elirinyo)

Kibao cha uzinduzi wa Kanisa la KKKT usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ilipofanyikia ibada ya mazishi ya Emmanueli Sabuni. (Picha na Elirinyo)

Gari lililoubeba mwili wa Marehemu Emmanuel Sabuni likiwasili katika Kanisa la KKKT usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ilipofanyikia ibada ya mazishi ya Emmanueli Sabuni. (Picha na Elirinyo)

Mdogo wake na marehemu aliyeshikilia msalaba akiwa tayari kwa kuingiza jeneza lililobeba mwili wa Marehemu kaka yake kanisani. (Picha na Elirinyo).

Kikundi cha "The Hopers" wasichana wakiwa tayari kuusindikiza mwili wa marehemu kuingia kanisani (Picha na Elirinyo).


Kikundi cha "The Hopers" wanaume wakiwa wamelibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu kuliingiza kanisani. (Picha na Elirinyo).


Mdogo wa marehemu akitoa maneno ya shukrani na ya msamaha kwa aliyesababisha kifo cha kaka yake baada ya risala kusomwa (Picha na Elirinyo).

Katika hatua nyingine mdogo wamarehemu kwa niaba ya familia ya Sabuni alitangaza msamaha wa dhati kwa aliyesababisha kifo cha kaka yake kwa ajali, jambo ambalo liliwafanya waombolezaji wengi kutokwa na machozi. 

Waombolezaji wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho (Picha naElirinyo).

Waombolezaji wakiwakatika hali za majonzi katika eneo la kanisa (Picha naElirinyo).

T-shirts zenye picha ya Emmanuel na mwenzake waliyefariki naye pamoja Carthbet ambaye atazikwa siku ya Jumatatu huko Moshi nazo zilitawala katika msiba (Picha naElirinyo).

Gari iliyobeba mwili wa marehemu ikisukumwa kutokana na kukwama kwenye tope baada ya mvua iliyonyesha katika eneo la makaburi ya Njiro (Picha naElirinyo).

Vijana wakianza kazi ya kuifukia nyumba ya milele ya marehemu Emmanuel Sabuni baada ya taratibu za kikanisa kufuatwa. (Picha naElirinyo).



Baba wa marehemu Bw. Robson Sabuni aliyevaa suti ya rangi ya maziwa akionekana mwenye huzuni katika eneo la makaburi ya Njiro baada ya kifo cha kijana wake mpendwa Emmanuel (Picha naElirinyo)..


Baba mzazi wa marehemu na mkewe wakiweka shada la maua katika nyumba yake ya milele (Picha na Elirinyo).


Bibi zake na Marehemu wakiweka shada la maua kama heshima ya mwisho (Picha naElirinyo).




Wazungu ambao ni rafiki zake na Emmanuel na walishawahi kufanya kazi pamoja wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Emmanuel (Picha naElirinyo).


Kiongozi wa Ibada Mwinjilisti Materu akitoa neno la shukrani na la mwisho makaburini (Picha naElirinyo).

Kaburi la Emmanuel kama linavyoonekana baada ya watu mbalimbali kuweka mashada yao ya heshima (Picha naElirinyo).

Waombolezaji walikumbwa na adha ya matope baada ya mvua iliyonyesha eneo la makaburini hivyo kusababisha baadhi ya magari kukwama na hapa baadhi ya waombolezaji wakiwa wanondoka makaburini baada ya maziko.(Picha naElirinyo).

Kumbuka:
Mwisho wa safari ya Emmanuel Robson Sabuni hapa Duniani ni mwanzo wa safari mpya ya Mbinguni, Bwana atoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe, Amen!!!!

@RINYO'S 

Wednesday, 9 December 2015

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA LEO HII KIMEKUMBWA NA SIMANZI KUBWA BAADA KUKUMBWA NA TANZIA YA VIJANA WAO WAWILI WA NGAZI YA SHAHADA (DEGREE).


Ulikua ni mchana mzuri wenye pilikapilika za hapa na pale huku ukihusisha pia maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambayo yaliambatana na tukio la kufanya usafi katika maeneo ya majumbani na kazini pia kama utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Lakini siku haikuweza kuisha vizuri katika Chuo cha Uhasibu Arusha kwani mnamo majira ya saa 11 jioni zilianza kusambaa taarifa za uvumi wa vifo vya wanafunzi wawili, huku wanafunzi wengi wakiwa katika kuhamaki na wakipambana huku na kule ili kuupata ukweli juu ya taarifa hizi ndipo taarifa rasmi zilipotufikia kuwa wanafunzi wawili wa ngazi ya Shahada wa chuo Cha Uhasibu Arusha wamepata ajali katika barabara ya Njiro - Arusha karibu na Kituo cha Mafuta cha BP. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa ajali hiyo ilihusisha Pikipiki iliyokuwa ikitumiwa na wanafunzi hao pamoja na gari aina ya Land Cruizer, mashuhuda wanadai kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Marehemu Carthbet Massawe iligongana na gari hilo na kusababisha ajali hiyo kutokea ambayo ilisababisha Carthbet kupoteza maisha hapohapo huku mwenzake ambaye ni Emmanuel Robson Sabuni akiwahishwa Hospitali kutokana na majeraha aliyoyapata lakini hata hivyo kwa taarifa tulizozipata kutoka Hospitali ni kuwa pia Emmanuel naye alifariki akiwa katika chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU).

Kwa kweli vifo hivi vimepokelewa kwa simanzi kubwa hapa chuoni huku wengi wakiwa bado hawaamini kwa taarifa wanazozipata kutoka kwa Magroup yao ya Whatssap ya madarasani. Vijana hawa wametutoka wakiwa bado wadogo sana huku wakikadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 23 na 25, Marehemu Emmanuel Sabuni alikua ni mwanafunzi wa Shahada ya TEHAMA (BIT) mwaka wa kwanza huku mwenzake ambaye ni Marehemu Carthbet Massawe akiwa ni mwanafunzi wa Shahada mwaka wa pili.

Wote walikua ni watumishi wa Mungu katika Fellowship ya ICF hapa chuoni na walikua katika maandalizi ya sherehe ya Kidini ya kuwakaribisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza (ICF FRESHERS) ambayo ilitarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Tarehe 12/12/2015.


Marehemu Emmanuel Sabuni katika enzi za uhai wake akiwa Madhabahuni.
Marehemu Emmanuel Sabuni akionekana katika moja ya Events alizoshiriki kuziandaa.
Marehemu Carthbet Massawe katika enzi za Uhai wake.
 Marehemu wote kwa pamoja wataacha pengo kubwa katika Fellowship ya ICF kwani walikua watu muhimu sana katika Team ya Maombi na Kwaya ya ICF, pia Marehemu Emmanuel ataacha pengo kubwa katika kanisa la KKKT alilokua anasali ambapo yeye alikua ni kiongozi wa kwaya.

Marehemu Carthbet Massawe na Marehemu Emmanuel Sabuni katika picha ya pamoja, Bwana ametoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe. R.I.P Brothers.


Share na wengine ili tuzidi kuwaombea wapendwa wetu hawa walazwe mahali pema peponi.

@RINYO'S

UKAWA WAJAZANA MAHAKAMA ZA KANDA YA ZIWA KUTETEA NAFASI ZAO ZA UBUNGE:



KESI za kupinga matokeo ya ubunge zimezidi kumiminika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ikiwamo za kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya (Chadema)
Kesi nyingine zilizofunguliwa mahakamani ni za majimbo ya Nyamagana, Ilemela na jimbo la Kwimba, ambapo walalamikaji wamewasilisha malalamiko mbali mbali ikiwamo ya vitendo vya rushwa.

Kesi ya kwanza iliyofunguliwa ni ya ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini ambayo imefunguliwa na Magambo Masato na wenzake watatu wakipinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2015 mara ya kwanza ilifunguliwa Novemba 18 mwaka huu, juzi ilikuwa mara ya kwanza kupelekwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa.

Kesi hiyo ambayo ipo kwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe, walalamikaji wa kesi hiyo wamewasilisha malalamiko mahakamani hapo wakidai kwamba Bulaya alipata ushindi kwa njia ya rushwa.

Bulaya aweka pingamizi
Mlalamikiwa katika kesi hiyo, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Ester Bulaya, mapema juzi aliwasilisha hoja za msingi kuweka pingamizi kwa walalamikaji kufungua kesi mahakamani.

Hoja alizowasilisha Bulaya ni kwamba walalamikaji hawana mamlaka ya kufungua na kuendesha kesi ya aina hiyo kwani hawajaonesha ni namna gani imeathiri haki zao kama wapiga kura.

Pili katika shauli walillowasilisha mahakamani hawakuonesha ni namna gani vitendo vya rushwa walivyodai vilikuwa vikifanywa na Mawakala wa Bulaya havijaoneshwa, pia shauri hilo limekiuka kifungu cha 12 (D) cha sheria ya uchaguzi.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 29 mwaka huu, itakapo tajwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya kuisikiliza.

Kesi ya Wenje
Aliyekuwa Mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiah Wenje, juzi alitinga Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, kuomba kupunguziwa gharama za uendeshwaji wa kesi.

Pia Wenje katika kesi hiyo anawashitaki, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM), Msimamizi wa Uchaguzi huo, Tito Mahinya na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo amewasilisha malalamiko mahakamani hapo kwamba uchaguzi huo haukuwa haki na huru, kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Hata hivyo katika kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2015, Wenje aliwakilishwa mahakamani hapo na Wakili Outa na upande wa walalamikiwa waliwakilishwa na Wanasheria wa Serikali, Mtalemwa, Kitia Tuloke na Ajuaye Bilishaga.

Kesi ya Highness Kiwia
Novemba 25 mwaka huu aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ilemela, Highness Kiwia, alifungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi, Angelina Mabula (CCM) pamoja na kuwashitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi huo, John Wanga.

Kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, mlalamikaji katika kesi Kiwia hakufika mahakamani hapo, ambapo kwa upande wa walalamikiwa waliwakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Malongo.

Kesi ya Wenje na Kiwia zimeahirishwa ampapo ya Wenje itatajwa Desemba 10 mwaka huu na ya Kiwia hadi Desemba 14 mwaka huu, huku Msajili, Kabwe amedai kuwa endapo siku hiyo mlalamikaji Kiwia hatatokea kesi itatupiliwa mbali.
 
 
@RINYO'S
LEO NI SIKU MUHIMU SANA KWA NCHI YETU KWA KUTIMIZA MIAKA 54 TANGU ILIPOJIPATIA UHURU WAKE MNAMO TAREHE 09/12/1961.


Lakini leo hii Rais wa Awamu ya Tano Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameamua watu wote waadhimishe siku hii kwa kufanya usafi katika makazi yao na maeneo yao ya kazi ili kuweza kukabiliana na Ugonjwa wa KIPINDUPINDU, zoezi hilo limeanza kutekelezwa asubuhi hii ya leo huku Mh. Rais akiliongoza kwa kufanya usafi katika eneo la Soko la Feri .

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Janeth akiongoza zoezi la kufanya usafi katika Soko la Feri.


Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongoza wananchi wa eneo chalinze kufanya usafi
Kama hiyo haitoshi pia wasanii na baadhi ya vituo vya Redio vikiongozwa na Clouds Media Group wameshiriki katika kufanya usafi ikiwa ni njia ya kutekeleza agizo la mheshimiwa Rais.



Watangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm #TeamLeoTena wakiwa katika mavazi ya usafi kwa ajili ya kulitimiza agizo la Rais. (Dahuu, Musa Husein, Jose Mara, Ge Habibu nk.)

Katika kufanya usafi huku kumeibua mengi hapa ni watangazaji wa Clouds Fm wakitoa meno ya Ng'ombe ambayo yalikua yamehifadhiwa kwa takribani miezi sita kwa bibi mmoja mkazi wa Tandale ambayo yalikua yakiwasababishia majirani kero.

Staa wa bongo Fleva Tundaman akiwa na Team Leo Tena ya Clouds wakifanya usafi eneo la Soko la Tandale.

Pia Taasisi mbalimbali zimeonyesha kuunga mkono kauli ya Rais ya kufanya usafi ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya SEKOTOURE iliyoko jijini Mwanza pia Taasisi za Elimu ya juu ikiwa ni pamoja na Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM nacho kimeunga agizo la Mh. Rais kwa asilimia 100 na katika mbao zake za matangazo kulisomeka hivi.

Tangazo katika mbao za matangazo za Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kama linavyoonekana.


Mwanafunzi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefahamika kwa jina moja la Shangwe akivaa Gloves tayari kwa kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la kufanya usafi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya SEKOTOURE Jijini Mwanza wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi tayari kutekeleza agizo la Rais.






Usisahau kutoa maoni yako juu ya maamuzi haya ya Rais na pia kuhusiana na mwitiko wa wananch katika eneo lako

@RINYO'S