Leo ilikua ni siku nyingine ya majonzi kwa Chuo cha Uhasibu Arusha kutokana na mazishi ya kijana wao mpendwa wa Shahada ya Uhasibu mwaka wa pili marehemu Curthbet Massawe, Marehemu alifariki katika ajali iliyohusisha pia kupoteza uhai wa kijana mwingine wa Uhasibu Marehemu Emmanuel Sabuni ambaye yeye alipumzishwa rasmi katika nyumba yake ya milele siku ya Jumamosi ya tarehe 12/12/2015.
Katika mazishi hayo yaliyoonekana kugusa watu wengi Chuo cha Uhasibu kikiongozwa na Mwadili wa wanafunzi (Matron) kilitoa jumla ya waombolezaji zaidi ya 350 ili kuwawakilisha wanafunzi wote katika kuifariji familia ya marehemu Curthbert Massawe.
Mazishi haya yalisababisha watu wengi kutokwa na machozi na wengine hata kupoteza fahamu hasa ukizingatia kuwa kijana alikua bado ni mdogo mno kwani amefariki akiwa na umri wa miaka 26 tu.
Mwili wa marehemu uliagwa rasmi katika Vyumba vya kuhifadhia maiti (Mouchwary) katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru majira ya saa tatu, na ndipo safari ya kuelekea Moshi ilipoanza ikijumuisha Coster 8 zilizobeba wanafunzi na magari mengine ya watu binafsi yapatayo 6, kabla ya safari kuanza ilifanyika sala ya kumuombea marehemu na pia kuibariki safari, pia baba na mama wa Marehemu Emmanuel Sabuni ambaye walipata ajali pamoja na Curthbet alitoa neno la faraja kwa wazazi wa Curthbet pamoja na kwa waombolezaji kisha akatutakia safari njema.
![]() |
| Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Tema akiweka shada pamoja na mchungaji mwenzake katika kaburi la Curthbet Massawe. (Picha na Elirinyo). |
![]() | |
|
![]() |
| Baba na Mama (Wazazi) wa Curthbet wakiweka shada katika kaburi la mwanao.(Picha na Elirinyo) |
![]() |
| Baba na Mama (Wazazi) wa Curthbet wakiweka shada katika kaburi la mwanao.(Picha na Elirinyo) |
![]() |
| Mwadili wa wanafunzi (Matron) katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) akiweka shada kwa niaba ya Management.(Picha na Elirinyo) |
![]() |
| Kaka zake na Curthbet wakiweka mashada katika kaburi la mdogo wao (Picha na Elirinyo) |
![]() |
| Mjomba akienda kuweka shada katika kaburi la marehemu (Picha na Elirinyo). |
![]() | |
|
![]() |
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen!!
@RINYO'S










No comments:
Post a Comment