Arsenal yazidi kuisogelea Leceister City kileleni..........Ozil azidi kungara EPL...........!!
Ikitumia vyema Uwanja wake wa nyumbani wa Emirates usiku wa Tarehe 21/12/2015 katika mwendelezo wa Ligi kuu nchini Uingereza timu ya Arsenal maarufu kama The Gunners imeweza kuifunga timu ya Manchester City kwa jumla ya magoli 2-1 na hivyo kuzidi kuipumulia klabu ya Leceister City ambao ndio vinara wa ligi.![]() |
| Theo Walcott akishangilia na Mesut Ozil baada ya kuipatia Arsenal goli la kwanza |
![]() |
| Wachezaji wa Arsenal wakipongezana baada ya kujipatia goli la kuongoza. |

Mvuto wa mchezo huu unakuja kutokana na
timu zote kuwa katika nafasi tatu za juu, hivyo ushindi kwa kila timu
ulikuwa ni muhimu kwani utakuwa unamuweka karibu na Leicester City inayoongoza. Kama hiyo haitoshi mnamo dakika ya 45 ya mchezo Olivier Girou alipokea pasi kutoka kwa Ozil tena na kuifungia Arsena goli la pili.
Hadi mpira unakwenda mapumziko ubao ulisomeka Arsenal 2-1 Manchester City.
![]() |
| Mshambuliaji Olivier Giroud akiifungia Arsenal goli la pili. |

Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake wa kifaransa Oliver Giroud alipachika wavuni goli la pili dakika ya 45 na kuufanya mchezo kumalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Man City, huku goli la Man City likifungwa na Yaya Toure dakika ya 82. Kwa matokeo hayo Arsenal wanakuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi wakiwa na jumla ya point 36 tofauti ya point 2 na Leicester City wanaoongoza Ligi.




No comments:
Post a Comment