RAIS WA TANZANIA Dr. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA MBALIMBALI LEO IKULU DAR ES SALAAM...................
Wakati watu wengi duniani kote wakiwa bize na sikukuu ya Mwaka mpya ambayo imekua ni sikukuu ambayo imekua ikiadhimishwa na familia nyingi ulimwenguni kwa kukaa na ndugu zao pamoja na jamaa na marafiki na kujumuika katika kusherehekea, leo Rais mpya wa Tanzania wa Awamu ya Tano ameenda tofauti kwa kuingia ofisini (Ikulu) na kuwaapisha Makatibu wakuu na manaibu wao wa Wizara mbalimbali na kuudhihirishia umma kuwa kweli "Hapa ni Kazi Tu".
Katika hafla hiyo Rais Dr. Magufuli amewaapisha Makatibu wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.
![]() |
| Ukumbi wa Ikulu ya Dar es Salaam kama unavyoonekana wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali na Manaibu. |
@RINYO'S




Thanks for visit my site
ReplyDelete