Saturday, 12 December 2015

MATUKIO:

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAFANIKIWA KUMZIKA EMMANUEL SABUNI SALAMA.

Leo katika eneo la Njiro kulikua na mazishi ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Marehemu Emmanuel Robson Sabuni ambaye alipoteza maisha siku ya Jumatano ya Tarehe 09/12/2015 kutokana na ajali iliyohusisha gari aina ya Land Cruiser na pikipiki waliyokua wakiitumia kusafiria kuelekea mjini ambapo katika ajali hiyo Emmanuel alikua pamoja na mwanafunzi mwenzake aitwaye Carthbet Massawe ambaye naye pia alipoteza maisha kutokana na ajali hiyo. 

Emmanuel amefariki akiwa na umri wa miaka 25 tu, ambapo alizaliwa mnamo Tarehe 25/05/1990 na kufariki Tarehe 09/12/2015 siku ya Jumatano. 

Baadhi ya waombolezaji wakiondoka nyumbani kwa mzee Robison Sabuni baba mzazi wa marehemu eneo la Kikokwaru (Double B) kuelekea kanisani ilipofanyika ibada ya maziko. (Picha na Elirinyo).

Baadhi ya waombolezaji wakiondoka nyumbani kwa mzee Robison Sabuni baba mzazi wa marehemu eneo la Kikokwaru (Double B) kuelekea kanisani ilipofanyika ibada ya maziko. (Picha na Elirinyo).

Ibada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ambapo Ibada iliongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika Mch. Letare, ambaye katika mahubiri yake aliwakumbusha wote waliohudhuria safari hiyo ya mwisho ya mpendwa wetu Emmanuel kujiweka tayari kwa ni kwani ni kwa wakati wowote tena tusiodhani tunaweza kukumbwa na mauti kwani kifo kimeumbiwa mwanadamu, Mch. Letare akitumia neno kutoka kitabu cha nabii Isaya 37:1-8 alisema ni wakati wa sisi kujikita katika kutenda mema ili hata wakati wa hukumu yetu tupate kumkumbusha Mungu kwa yale mema tuliyokwisha kuyafanya kama alivyofanya Mfalme Hezekia.


Lango kuu la kuingilia Kanisa la KKKT usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ilipofanyikia ibada ya mazishi ya Emmanueli Sabuni. (Picha na Elirinyo)

Kibao cha uzinduzi wa Kanisa la KKKT usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ilipofanyikia ibada ya mazishi ya Emmanueli Sabuni. (Picha na Elirinyo)

Gari lililoubeba mwili wa Marehemu Emmanuel Sabuni likiwasili katika Kanisa la KKKT usharika wa Kijenge mtaa wa Sayuni Njiro ilipofanyikia ibada ya mazishi ya Emmanueli Sabuni. (Picha na Elirinyo)

Mdogo wake na marehemu aliyeshikilia msalaba akiwa tayari kwa kuingiza jeneza lililobeba mwili wa Marehemu kaka yake kanisani. (Picha na Elirinyo).

Kikundi cha "The Hopers" wasichana wakiwa tayari kuusindikiza mwili wa marehemu kuingia kanisani (Picha na Elirinyo).


Kikundi cha "The Hopers" wanaume wakiwa wamelibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu kuliingiza kanisani. (Picha na Elirinyo).


Mdogo wa marehemu akitoa maneno ya shukrani na ya msamaha kwa aliyesababisha kifo cha kaka yake baada ya risala kusomwa (Picha na Elirinyo).

Katika hatua nyingine mdogo wamarehemu kwa niaba ya familia ya Sabuni alitangaza msamaha wa dhati kwa aliyesababisha kifo cha kaka yake kwa ajali, jambo ambalo liliwafanya waombolezaji wengi kutokwa na machozi. 

Waombolezaji wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho (Picha naElirinyo).

Waombolezaji wakiwakatika hali za majonzi katika eneo la kanisa (Picha naElirinyo).

T-shirts zenye picha ya Emmanuel na mwenzake waliyefariki naye pamoja Carthbet ambaye atazikwa siku ya Jumatatu huko Moshi nazo zilitawala katika msiba (Picha naElirinyo).

Gari iliyobeba mwili wa marehemu ikisukumwa kutokana na kukwama kwenye tope baada ya mvua iliyonyesha katika eneo la makaburi ya Njiro (Picha naElirinyo).

Vijana wakianza kazi ya kuifukia nyumba ya milele ya marehemu Emmanuel Sabuni baada ya taratibu za kikanisa kufuatwa. (Picha naElirinyo).



Baba wa marehemu Bw. Robson Sabuni aliyevaa suti ya rangi ya maziwa akionekana mwenye huzuni katika eneo la makaburi ya Njiro baada ya kifo cha kijana wake mpendwa Emmanuel (Picha naElirinyo)..


Baba mzazi wa marehemu na mkewe wakiweka shada la maua katika nyumba yake ya milele (Picha na Elirinyo).


Bibi zake na Marehemu wakiweka shada la maua kama heshima ya mwisho (Picha naElirinyo).




Wazungu ambao ni rafiki zake na Emmanuel na walishawahi kufanya kazi pamoja wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Emmanuel (Picha naElirinyo).


Kiongozi wa Ibada Mwinjilisti Materu akitoa neno la shukrani na la mwisho makaburini (Picha naElirinyo).

Kaburi la Emmanuel kama linavyoonekana baada ya watu mbalimbali kuweka mashada yao ya heshima (Picha naElirinyo).

Waombolezaji walikumbwa na adha ya matope baada ya mvua iliyonyesha eneo la makaburini hivyo kusababisha baadhi ya magari kukwama na hapa baadhi ya waombolezaji wakiwa wanondoka makaburini baada ya maziko.(Picha naElirinyo).

Kumbuka:
Mwisho wa safari ya Emmanuel Robson Sabuni hapa Duniani ni mwanzo wa safari mpya ya Mbinguni, Bwana atoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe, Amen!!!!

@RINYO'S 

No comments:

Post a Comment