Friday, 8 January 2016

BAADA YA TUZO SAMMATA SAMMA GOAL "GOLDEN BOY WA BONGO" KUTUA SAA SITA USIKU...........

Mbwana Ally Sammata Mtanzania aliyeweza kuweka Rekodi kwa wanasoka wote wanaosukuma kandanda katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa mwanasoka wa kwanza kutoka Bongo kuichukua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wanaocheza nyumbani Afrika.
Ikumbukwe pia Sammata anaitumikia pia Klabu bingwa ya Afrika TP Mazembe ya DRC Congo. Na katika tuzo hii alikua akiigombea tuzo hii na mchezaji mwenzake wa TP Mazembe golikipa Robert Kidiaba ambaye aliibuka mshindi wa pili.
Mbwana Ally Sammata akiipokea Tuzo yake ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka Afrika tu.
 Sammata atatua usiku wa leo na kupokelewa na wadau mbalimbali ambao wameguswa na tuzo hii. Wadau mbalimbali wa soka wamejichanga kwa kuandaa tafrija fupi ya kumpongeza itakayofanyika Escape One chini ya usimamizi wa Clouds Media Group na wadau wengine wa soka


Sammata shujaa akiwa amelala na Tuzo yake huku akiwa amejifunika na Bendera ya Taifa.

Mbwana Sammata amepokea salamu mbalimbali  za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali akiwamo pia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kupitia kwa waziri wa Michezo Mh. Nape Nauye.
Pia Viongozi mbalimbali akiwemo Mh. Zitto Kabwe, mastaa mbalimbali kama Diamond na Jackline Wolper pia wamempongeza katika page zao za mitandao ya kijamii.

##vivaSammata-thatIsWhatIcan-Say###

Karibu nyumbani Shujaaaa!!!!!

@RINYO's 

1 comment: