Sunday, 31 January 2016

ZIARA YA WAZIRI MKUU YA KUSHTUKIZA:

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.




Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  picha za mionzi (X Ray) katika hospitali  ya rufaa  ya Mawenzi.
Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro, Dkt Mtumwa  Mwako.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo , Mhe. James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi.                                       

KITAIFA.

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA LEO IKULU DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Dkt. 
Mahadhi Juma Maalim baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo baada ya kumuapisha  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve bvaada ya kumuapisha  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kabla ya  kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Kamishna wa Polisi  Paul Amani Moses Chagonja baada ya kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 
 
 
@RINYO'S

Sunday, 24 January 2016

MATUKIO CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

TOP FIVE HABARI KUBWA ZA WIKI (IAA):



1: KUZINDULIWA KWA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA IAASO:

Tarehe 19/01/2016.

Kampeni rasmi za uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri mkuu zinazinduliwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha baada ya kukwamishwa na pingamizi lililokuwa limewekwa kwa mmoja wa wagombe mmojawapo wa kiti cha Urais Ndg. Reginald Massawe, ambapo alifanikiwa kushinda pingamizi hilo ambalo lilitolewa maamuzi yake mnamo siku ya Jumatatu Tarehe 18/01/2016 kwenye mishale ya saa Mbili usiku.

Mgombea wa Urais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha Bw. Reginald Massawe aliyekuwa amewekewa pingamizi hapo awali.


2: PICHA ZA WAGOMBEA ZAWEKWA NA KUSAMBAZWA KWENYE MBAO MBALIMBALI ZA MATANGAZO:

 (A.) Wagombea watatu wa ngazi ya Urais ambao ni MASSAWE REGNALD, ZUBERI MAHAMUDU na SAID:

Wagombea wa nafasi ya Urais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO).


(B.) Wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais walikua ni MWIGUNE ESTER na KATUNZI FARIDA.

Wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO)

(C.) Wagombea wa nafasi ya Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) walikua ni ELIBARIKI BONIFACE, MBOTOYO EMMANUEL na ALFA MAHAMED.

Wagombea wa nafasi ya Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO)


 3: KAMBI MBILI ZAIBUKA RASMI WAKATI WA KAMPENI:

 Kweli wahenga walisema siku zote  maji hujitenga na mafuta, na ndivyo ilivyokuwa kwenye kampeni za uchaguzi huu ambapo kuliibuka kambi mbili zilizoibua ushindani mkubwa katika uchaguzi huu haswa wakati wa kampeni ambapo kambi hizo zilikua ni kambi ya Team Massawe na Team Mahamudu ambapo hizi kambi mbili zilihusisha viongozi wa nyazifa zote tatu, namaanisha nyadhifa za Urais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Huku kambi ya Team Massawe ikiwa na Massawe mwenyewe, Ester Mwigune na Elibariki Boniface, Upande wa pili wa Team Mahamudu ulikua na Mahamudu Zuberi, Katunzi Farida na Mbotoyo Emmanuel.

Kambi ya Massawe Regnald
 Kambi ya Massawe Regnald ilikua inajinadi kwa kutumia Ilani yao inayosema "Accountable, Transparent and Responsible Leadership" wakimaanisha "uongozi wa Uwajibikaji na uwazi".


Kambi ya Mahamudu Zuberi


Kambi ya Mahamudu Zuberi ilikua ikijinadi kwa Ilani yao inayosema "You Are the Best, Choose the Best, Hope for All" wakimaanisha "Wewe ni Bora, Chagua kilicho Bora, Tumaini la Wote".

Wagombea wawili pekee ndio waliokuwa binafsi na walikua na kambi huru ambao ni Said Mgombea wa nafasi ya Rais na Alfa Mohamed aliyekua mgombea wa nafasi ya Waziri Mkuu.

Kampeni za uchaguzi huo wa viongozi wa IAASO zilizidi kushika kasi kati siku ya pili ambayo ni Jumatano ambapo pia zilikumbwa na vikwazo vya hapa na pale ikiwamo pia mvua iliyozuia wagombea kutoka darasa moja hadi jingine huku pia madarasa kuwa na wanafunzi wachache.


5: UCHAGUZI WAFANYIKA NA MATOKEO YATANGAZWA:


Tarehe 22/01/2016.

 Siku ya Ijumaa ya Tarehe 22/01/2016 ndo siku iliyokuwa muhimu baada ya kampeni zilizodumu kwa takribani masaa 72. Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha walitakiwa kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wao wa serikali ya wanafunzi ya wanafunzi (IAASO), Siku ilikua imetulia sana huku kukiwa na pitapita za hapa na pale pia kukihusisha vikundi vidogo vidogo vya wanafunzi hapa na pale wakitoa mitazamo tofauti juu ya wagombea baada ya kupiga kura zao.

Zoezi liliendelea hivyo hadi saa 10:30 Jioni ambapo vituo vilisitisha zoezi la kupiga kura na kuanza zoezi jipya la kuhesabu kura na kisha kuzipeleka kura katika kituo kikuu ambapo yalifanyika Majumuisho.

Huku watu wengi wakiwa na hamu kubwa kusikia matokeo na kujua kipi hasa kimetokea ndipo Mwenyekiti wa Tume alipotoka na kutangaza matokea ambayo yalionyesha kuwa Bw. Massawe Regnald aliibuka mshindi wa kiti cha Urais kwa kupata jumla ya Asilimia 77.7% ya kura zote zilizopigwa huku akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu Bw. Mahamudu Zuberi aliyejipatia Asilimia 21.58%.

Kwa upande wa Makamu wa Rais Mwigune Ester aliibuka mshindi kwa kujipatia ushindi wa Asilimia 71.07% huku mpinzani wake Katunzi Farida akijipatia Asilimia 28.92%.

Katika matokeo ya Waziri Mkuu kulikua na mchuano kidogo ambapo wagombea watatu waligawana kura na mwisho Bw. Elibariki Boniface aliibuka kidedea kwa Asilimia 59.75% huku mpinzani wake wa karibu Bw. Alfa Mohamed akipata Asilimia 27.29% na Mbotoyo Emmanuel akipata Asilimia 12.95%.

Matokeo ya Uchaguzi wa IAASO katika Picha (Picha na Elirinyo)

JICHO LA MWEWE LA MPEKUZI RINYO:

MAPUNGUFU:

Kwa kweli uchaguzi huu umegubikwa na Mapungufu kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na 

 - Mwamko mdogo wa wapiga kura
Chuo cha Uhasibu kwa makadirio ya chini kabisa kina Idadi ya wanafunzi Takribani 3000 (Elfu tatu) hayo ni makadirio ya chini kabisa lakini idadi ya waliopiga kura jumla ni wanafunzi 1455. unaona ni kwa namna gani mwamko ni mdogo kiasi cha kutokufikia hata nusu ya makadirio.

- Tume kutokuwa na karatasi maaalum za kufanyia mjumuisho wa matokeo. Kwa jicho langu la mwewe nimeweza kugundua kabisa karatasi iliyotumika kujumuishia matokeo ya ujumla kabisa ilitengenezwa kwa kutumia Rula na Kalamu jambo ambalo ni hatari sana kwani mtu yeyote anaweza akatengeneza matokeo kisha akabandika kabla ya Tume.

- Tume kutokuchukua hatua mathubuti kwa kampeni chafu na za kiholela zinazofanyika nje na ndani ya chuo, jambo ambalo linaweza kuchangia machafuko chuoni na hata kupandikiza chuki za kudumu baina ya wanafunzi.

- Jicho la Mwewe pia limeona mapungufu katika muda wa kufanya kampeni 

MAONI YA MPEKUZI RINYO:

- Tume zijazo lazima zianzishe utaratibu mpya au mfumo mpya wa kuwagusa kila wanafunzi na kuwajengea hamasa za kushiriki katika uchaguzi hasa wanaume.

- Tume inatakiwa kuandaa na kuzifuatilia sheria na kanuni zake vizuri ili kuweza kuepuka vitendo vya kampeni chafu dhidi ya wagombea



 @RINYO'S



 

MATUKIO YA WIKI KITAIFA:

1. RAIS MAGUFULI AZIDI KUWA GUMZO NCHINI:




Mnamo Tarehe 20/01/2016 Mh. Dkt. John Pombe Magufuli anaonyesha ujuzi wake wa kutumia Cherehani
 

ANGALIA PICHA ZA RAIS DR. MAGUFULI AKISHONA NGUO KWA CHEREHANI...!!!


 Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherehani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali na watumishi wake wa  Ikulu jijini Dar es salaam jana Januari 20, 2016.
 


2: WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BUNGE LA AWAMU YA TANO DODOMA:

Tarehe 22/01/2016

Kwa mara nyingine tena shughuli za Bunge zinaanza upya baada ya kufunguliwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016.  Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kahilillah
 Wabunge, Jenista Mhagama wa Peramiho (kushoto) na January Makamba  wakiteta katika mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerge Masaju akitoa mada katika mkutano wa wabunge , bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016.


 Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkutano wa Wabunge, Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kufungua mkutano huo bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016.


3: RAIS MH. MAGUFULI ATINGA MAGWANDA YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) AKIWA JIJINI ARUSHA:

Tarehe 22/01/2016.

Tukio hili lilizua gumzo kubwa sana mitandaoni na hii ni baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kuamua kuvaa mavazi ya kijeshi alipokua kwenye ziara yake Jijini Arusha. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma bango alilokabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech. Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
 Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.


4: ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA BARA LA AFRIKA DR. SALIM AHMED SALIM AZINDUA KITABU: 



Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia), na Mwakilishi wa Kituo cha Kutatua Migogoro Barani Afrika, (Centre for Humanitarian Dialogue-CHD), Bw. Mohamed Omary wakionyesha Fremu yenye Mashairi ya kumsifu Dkt. Salim, huku Waziri Mahiga akishuhudia tukio hilo.
Hivi ndivyo uso wa kitabu hicho unavyoonekana.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Dkt. Salim Ahmed Salim (Salim Ahmed Salim: Son of Afica),akimzungumzia historia iliyotukuka ya Dkt. Salim Ahmed Salim, kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho.

Dkt. Salim Ahmed Salim, akitoa maneno ya Shukrani kwa heshima aliyopewa kwa Mwandishi wa kitabu hicho lakini kwa wadau wote waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu chake. Aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (Katikati), akiwa na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho. 
 
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Dkt. Salim.

5: RAIS MH. MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JESHI HUKO MONDULI:

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili  katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.




 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.



 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia gwaride lililokuwa likipita mbele yake  kutoa heshima.


 Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli .
@RINYO'S