Sunday, 24 April 2016

KUMBUKUMBU CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

MIAKA MIWILI BAADA YA KIFO CHA HENRY KOGA....NA VURUGU CHUONI,


Ni takribani miaka miwili sasa imekatika baada ya Vurugu na Maandamano kuibuka katika Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA na hii ilikua ni baada ya kifo cha Mwanafunzi wa Chuo hicho Marehemu Henry Koga aliyeuawa kwa kuchomwa kisu usiku wa kuamkia tarehe 24/04/2013 alipokua akitokea maeneo ya chuo baada ya kujisomea.


Henry Koga wakati wa uhai wake.


Lilikua ni tukio lililogusa hisia za watu wengi sana hasa wanafunzi wa Chuo kizima na Asubuhi ya siku iliyofuata wanafunzi karibia wote kwa makadirio ni kama 80% ya wanafunzi wote walikusanyika kwa pamoja katika eneo la Freedom Square wakiadhimia kuandamana hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Arusha kwa dhumuni la kujua hatma zao za Usalama wao baada ya kutokea kwa vitendo vya ukabaji wa wanafunzi na kuporwa kwa mali zao pamoja na uvamizi wa hosteli na kuibiwa mali zao na tukio la kuchomwa kisu kwa mwanafunzi mwenzao pia likawa chagizo kubwa la kutaka kujua hatma ya usalama wao.

Elirinyo huyu hapa akisimulia kile alichokishuhudia siku hiyo-

"Kiukweli mimi nilifika chuoni kama kawaida lakini sikua najua kama ishu ilikua serious kivile maana nilikuta wanafunzi weeengi wamejikusanya pamoja katika vikundivikundi wakijadili kuhusu kuandamana....ninachokumbuka ni kuwa nilifika wakati Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Kamanda Liberatus Sabasi ndiye alikua juu ghorofani akiongea na wanafunzi kwa kuwafariji lakini kuna kauli aliitoa ya kufananisha tukio hili na tukio lililotokea Zanzibar la kuuawa kwa Askofu Mushi pengine naweza kusema lile lilikua ndo kosa kwani niliwasikia wanafunzi kwa sauti za juu wakishout.....'Inahusiana na nini...Inahusiana na nini....inahusiana na nini' kelele hizi zilimfanya kamanda kushuka jukwaani, ndipo alipopanda Rais wa serikali ya Wanafunzi wawakati huo Bw, Benjamin Simkanga kuwatuliza wanafunzi kwa hekima lakini wanafunzi wakamzomea na kumwambia yuko upande wa Utawala na hataki wapate haki yao......kwa kweli hali ilikua mbaya sana na nilishaiona hali ya hatari, niliamua kuondoka eneo la tukio na kwenda kurejesha kitabu Maktaba kuepuka faini maana ilikua ndo siku ya mwisho, nilikua na matarajio ya kurejea eneo la tukio kuona nini kitaendelea lakini sikuweza kwani kuna muhudumu mmoja wa Maktaba alinishauri na kuniambia nibaki Maktaba maana hali itabadilika punde na kuwa mbaya nami nilitii ombi lake na kusalia maktaba"

-Elirinyo anatujuza nini hasa kiliendele-

"Japo nilikua Maktaba lakini kwa mbaali niliweza kuona wanafunzi wakiongozwa na Mbunge wa Arusha wakiandamana kuelekea katika ukumbi mkubwa wa Main Cafeteria huku wakiimba wimbo wa "Tunatakaaa haki zeetuu ....Tunataaaaka haki zeetu' na hii ni baada ya kuwasili kwa mkuuu wa Arusha wa wakati huo amabye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo......baada ya hapo nilikuja kujionea tuu kile kilichojiri kupitia video clip mbali mbali ambapo wanafunzi walidiriki kumfanyia fujo Mkuu wa Mkoa kwa kumrushia chupa za maji ndipo Jeshi la Polisi likaingilia kati na kumuondoa mkuu wa mkoa kwa usalama zaidi na kuanza kufyatua mabomu ya machozi....sisi tuliokuwa Maktaba hatukuweza kudhurika hata kidogo lakini waliokua nje ilikua ni mtafutano watu wakihaha huku na huko kusalimu maisha yao huku wengi wakipoteza mali zao mbalimbali ikiwemo simu, Laptops huku pia watu wa huduma za vinywaji wakipata hasara pia kutokana na vinywaji kuchukuliwa bila kulipiwa"

-Allan Zomanya alikua ni muathirika wa Mabomu ya machozi na hapa anaelezea-

"Kwa kweli mimi hapo awali nilikua silijui kabisa bomu la machozi likoje baada ya mabomu kuanza kupigwa nilikimbia na kujificha kwenye maua nyuma ya Main Cafeteria nikafanikiwa kuona kitu flani cha rangi ya silver lakini ghafla kilianzza kutoa moshi ndipo nilipoanza kuwashwa na macho nilikua nimevaa miwani na kutokana na muwasho nilichanganyikiwa na kuanza kukuna juu ya kioo cha miwani badala ya kutoa miwani ndo nijikune, kiukweli nilianza kuhisi kuishiwa nguvu ndipo nilipoamua liwalo na liwe nikaanza kukimbia kuelekea Administration nikarushiwa bomu la machozi jingine kwa mbele lakini nilibadili tu njia ila siyo kurudi....kingine nilichoshuhudia cha kusikitisha ni mdada aliyetaka kuruka mtaro kwa bahati mbaya akaishia kuanguka humo na kutupiwa bomu la machozi pale pale alipo...kwa kweli nilikimbia sana hadi Administration na kutafuta maji katika vyoo.."

Wanafunzi wengi wa Hostel walpata shida sana kwani mabomu yalikua yakirushwa katika Korido na kusambaa humo ndani...kunawanafunzi kadhaa waliokamatwa na Polisi na hii yote ilikua ni kwa ajili ya Kifo cha mwenzetu. ilikua mbaya sana wengi waliumia na kupoteza vitu vyao.

Tamko latolewa na Jeshi la Polisi tamko la kufungwa kwa chuo. Baada ya tamko hilo ulifuatia utekelezaji kwani matangazo yalibandikwa maeneo mbalimbali kama Hostel, Mbao za matangazo na Magetini ambapo tangazo lilikua likiamuru wanafunzi kutokuonekana eneo la chuo baada ya Masaa mawili huku tangazo likitolewa saa kumi kamili jioni.....ulikua ni wakati mgumu sana kwa dada zetu kwani wengine hawakua hata na Nauli na wengine kwao ni mikoa ya mbali na hawana ndugu Arusha......unataka kujua walikwenda wapi?.....

Baada ya hapo chuo kilifungwa kwa muda usiojulikana na kwa kipindi hiko tulikua tukijiandaa na Mitihani ya Final lakini ndo hivyo mambo yakabadilika, tuliweza kukaa nyumbani kwa kipindi cha mwezi mmoja mzima, tulirejea chuoni kwa barua kutoka kwa wakuu wa wilaya tunazoishi na pia kujisajilia upya Getini huku pia tukisaini fomu ya mkataba wa kutojihusisha na fujo zozote tuwapo chuoni


Tulifuatilia kujua chanzo cha kifo  cha mwenzetu lakini hadi leo hatujajua ni kipi hasa....Pumzika kwa amani Henry Koga.

MATUKIO KATIKA PICHA:


Henry Koga enzi za uhai wake

Henry Koga enzi za uhai wake

Henry Koga enzi za uhai wake

Mojawapo kati ya Post zilizosalia katika Account yake ya Facebook baada ya kifo chake

Mojawapo kati ya Post zilizosalia katika Account yake ya Facebook baada ya kifo chake

Mojawapo kati ya Post zilizosalia katika Account yake ya Facebook baada ya kifo chake
REST IN PEACE Henry Koga wanauhasibu tunakumiss....kwa kukumbushia ni kua wakati anafariki alikua ndiyo Current Mr. IAA.

@RINYO's


Sunday, 3 April 2016

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

 IAASO YATANGAZA BEI MPYA ZA STATIONARY .....NA PUNGUZO LA 50%...


Na Elirinyo Uronu

Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAASO) kupitia kwa Waziri Mkuu wake Bw. Boniface Elibariki yatangaza rasmi kupunguza bei za Stationary Chuoni hapo. Akitoa tangazo hilo waziri mkuu wa Serikali hiyo ameeleza kuwa wamefanya hivyo ikiwa ni katika kutimiza moja kati ya ilani na ahadi walizokuwa wanazitoa wakati wa kampeni za kuomba ridhaa ya kuongoza chuoni hapo.

Bw. Boniface Elibariki ametanabaisha kwamba hatua hiyo itawawezesha wanafunzi kuweza kumudu gharama za maisha chuoni hapo ikiwa ni pamoja na gharama hizo za Stationary.

katika taarifa hiyo inaonyesha kuwa Bei za Kuchapa (Printing) zimeshuka kwa asilimia takribani 50% kutoka Tsh. 200/= hadi Tsh. 100/= kwa ukurasa huku gharama za kutoa nakala (Photocopying) zikishuka pia kwa assilimia 50% kutoka Tsh. 50/= kwa kurasa hadi Tsh. 25/=

Tangazo la bei mpya za Uchapaji na kutoa Nakala kama linavyoonekana

@RINYO's